IQNA

Wanfunzi wa kike chuo kikuu Uganda wataka maafisa usalama wa kike

19:07 - December 08, 2021
Habari ID: 3474654
TEHRAN (IQNA)- Wanafuzni Waislamu katika Chuo Kikuu cha Kyambogo mjini Kampala nchini Uganda wanataka chuo hicho kiwaajiri maafisa usalama wanawake wanawake ambao watakua na jukumu la kuwapekua wanafunzi wa kike.

Ombi hilo limekuja baada ya afisa polisi mwanamume  kuwalazimisha wanafunzi Waislamu wa kike kuvua Hijabu zao ili wapekuliwe kabla ya kuingia katika chumba cha mitihani.

Kitendo cha afisa huyo wa polisi kiliwakera sana wanafunzi wa kike Waislamu na jamii ya Waislamu wa Uganda kwa ujumla. Sheikh Bakhit Cucu, Katibu wa Elimu katika Baraza Kuu la Waislamu Uganda (UMSC) amesema kitendo cha afisa huyo wa polisi ni ukiukwaji wa uhuru wa kuabudu katika katiba ya Uganda.

Amesema inapaswa kufahamika kuwa, kumvua mwanamke Mwislamu mtandio au Hijabu ni sawa na kumvua mavazi yake yote na hivyo yeyote anayefanya kitendo kama hicho anakuwa anamdahlilisha.

Hivi karibuni katika chuo hicho, mwanafunzi wa kike Aisha Nanfuma alzuiliwa kuingia chuoni hapo baada ya kusisitiza kuwa hatavua mtandio wake kama alivyotakiwa kufanya mbele ya afisa usalama mwanamume aliyekuwa akifanya upekuzi.

Aidha Sumaye Nakawesi, anayesomea taaluma ya uhasibu anasema chombo cha kupekua mwili kilipitishwa juu ya kichwa chake kwa sababu tu alikuwa amevaa mtandio ilihali wasiokuwa Waislamu waliokuwa wamevaa kofia hawakuwa wanapekuliwa kwa njia hiyo ya udhalilishaji.

Naye Halima Namuddi ambaye alidhalilishwa na maafisa usalama kutokana na Hijabu yake anasema jambo hilo lilikuwa na taathira hasi katika mtihani wake.

Wakati huo Naibu Kansela wa Chuo Kikuu cha Kyambogo Professor Eli Katunguka ametoa taarifa na kulaani udhalilishaji huo wa wanafunzi Waislamu na kusema haafiki jambo hilo.  Pamoja na hayo, Bashir Lule, mwenyekiti wa Jumuiya ya Waislamu katika Chuo Kikuu cha Kyambogo amesema uongozi wa chuo unapuuza malalamiko ya Waislamu. Amesema kuna haja ya kuchukua hatua za kivitendo za kuzuia kukaririwa vitendo hivyo na amependekeza kuwa maafisa usalama wanawake wapewa jukumu la kuwapekua wanafunzi Waislamu.

4018869

Kishikizo: waislamu uganda hijabu
captcha