IQNA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu

Umoja ni silaha pekee ya kukabiliana njama dhidi ya Uislamu

20:00 - December 28, 2021
Habari ID: 3474733
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema kuwa, umoja na mshikamano wa Waislamu ndiyo silaha pekee inayoweza kutumiwa kwa ajili ya kupambana na njama zinazofanywa dhidi ya Uislamu.

Hujjatul Islam wal Muslimin Hamid Shahriyari ameuambia mkutano wa Umoja wa Kiislamu uliofanyika mjini Islamabad Pakistan kwamba, Waislamu wanapaswa kuzika hitilafu zao, kwani siri ya mafanikio yao ni kujiepusha na uchochezi wa hitilafu na migawanyiko.

Shahriyari ameongeza kuwa, Waislamu wanaweza kuunda muungano wa nchi za Waislamu kwa utangamano, mshikamano na kujiepusha na makabiliano.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Pamoja Madhehebu za Kiislamu amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanya jitihada kubwa sana kwa ajili ya kupanua na kuimarisha zaidi umoja na mshikamano baina ha Waislamu.

Cleric Names Unity as Sole Weapon for Confronting Anti-Muslim Plots

Balozi wa Iran nchini Pakistan, Sayyid Muhammad Hosseini pia alihutubia mkutano huo ambapo amelaani hujuma na propaganda chafu dhidi ya Uislamu na kusema, umoja na juhudi za kukururbisha pamoja madhehebu za Kiislamu ni mambo mawili muhimu ya uokovu wa Umma wa Waislamu mkabala wa njama zinazofanywa na maadui yao.

3477124

captcha