IQNA

Ismail Haniya

Jinai za Israel haziwezi kusimamisha mapambano ya taifa la Palestina

11:19 - February 11, 2022
Habari ID: 3474916
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema mrengo wa muqawama au mapambano utalipiza kisasi cha damu za vijana watatu wa Kipalestina waliouawa shahidi hivi karibuni na jeshi katili la utawala haramu wa Israel.

Ismail Haniya sanjari na kutoa mkono wa pole kwa familia za mashahidi hao, amesisitiza kuwa hakuna shaka kwamba mauaji ya vijana hao wa Kipalestina mjini Nablus yatajibiwa.

Haniya ameeleza bayana kuwa, jinai hiyo ya kihaini ni sera iliyofeli na kugonga mwamba, na katu haiwezi kusimamisha nguvu za muqawama wa taifa la Palestina.

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya HAMAS ameongeza kuwa, makundi yote ya muqawama yanahisi kuwa yana wajibu na jukumu la kulipiza kisasi cha mauaji hayo ya kikatili.

Vijana hao watatu wa Kipalestina waliuawa shahidi siku chache zilizopita katika operesheni ya wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Makhfeya mjini Nablus, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibu wa Mto Jordan.

Misimamo ya kulaani jinai hiyo ya Nablus imetolewa pia katika ngazi ya kimataifa. Japokuwa madola yanayodai kutetea haki za binadamu duniani, kama kawaida yao, yamesalia kimya bila kuchukua hatua yoyote mkabala wa jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni, lakini taasisi na mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani yameitaja jinai hiyo ya Israel kuwa ni sawa na Apartheid. Wakati huohuo mitandao, mashirika ya haki za binadamu na jumuiya 277 za kiraia kutoka nchi 16 za Kiarabu na 6 za Ulaya na Amerika ya Latini zimesaini taarifa ya pamoja na kutahadharisha kuhusu sera za apartheid na ubaguzi za utawala wa Kizayuni na kutoa wito wa kuanzishwa kampeni ya kimataifa kwa ajili ya kutokomeza utawala kibaguzi wa Israel.  

3477765

captcha