IQNA

Msikiti mwingine wahujumiwa Canada

23:59 - March 19, 2022
Habari ID: 3475054
TEHRAN (IQNA)-Msikiti wa Masjid-an-Noor katika Mji wa St. John wa Canada uliharibiwa na kundi la watu wanaoaminika kuwa wabaguzi wenye chuki dhidi ya Uislamu siku ya Jumanne usiku.

Mwanachama mmoja wa msikiti wa St. John aliachwa "ametikiswa kabisa" wakati Msikiti wa Masjid-an-Noor ulipohujumiwa wakati wa ibada Jumanne, amesema mkuu wa Jumuiya ya Waislamu ya  Newfoundland na Labrador.
Tukio hilo lilitokea kabla ya saa 9:30 Jumanne usiku, alisema Syed Mansoor Pirzada.
"Alisikia kishindo kikubwa kwenye dirisha la upande. Ni wazi alianza na kutikiswa, kwa hivyo akatazama kwenye mfumo wa kamera na akaona watu watatu wakikaribia kutoka kwa lango la mbele," Pirzada alisema Ijumaa. "Walikwenda kwenye dampo la taka na wakaleta taka na kuzitupa mbele ya mlango."
Pirzada alisema kundi hilo pia lilinaswa kwenye kamera wakitupa mayai na vinywaji kwenye jengo hilo kabla ya kukimbia kuelekea Barabara ya Portugal Cove.
"Lilikuwa tukio la kushangaza sana kwetu sote," alisema.
Pirzada alisema mtu aliyekuwa ndani ya msikiti alikuwa na hofu. Aliashiria matukio mawili ya hivi majuzi ya mauaji ambayo ya ukatili dhidi ya Waislamu - ufyatuaji risasi katika msikiti wa Quebec ambao uliua watu sita mnamo Januari 2017, pamoja na mauaji ya watu wanne wa familia ya Pakistani-Canada ambayo yalihusisha mtu kugonga lori lake kwenye barabara kuu mnamo Juni 2021 ilipokuwa ikitembea familia hiyo. – matukio hayo yangali katika kumbukumbu za Waislamu.
Mwezi Januari Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau alitangaza kuwa chuki dhidi ya Uislamu ni jambo lisilokubalika na ameapa kuwa atahakikisha Canada ni nchi salama kwa Waislamu. Aidha amesema katika mpango wake wa kuangamia chuki dhidi ya Uislamu atateua mjumbe maalumu wa kukabiliana na tatizo hilo.
Mwaka jana serikali ya Canada ilitangaza Januaria 29 kuwa Siku ya Kitaufa ya Kukumbuka Hujuma dhidi ya Msikiti wa Quebec ambayo pia ni Siku ya Kukabiliana na Chuki Dhidi ya Uislamu.
Kwa mnasaba wa siku hii mwaka huu, serikali ya Canada imetoa taarifa na kusema inasimama pamoja na Waislamu nchini humo katika kukabiliana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Uislamu ni dini inayoenea kwa kasi zaidi Canada ambapo Waislamu wameongezeka kwa asilimia 82 katika kipindi cha muoongo moja uliopita. Hivi sasa Waislamu ni karibu asilimia 3.5 ya watu wote milioni 38 nchini Canada.
 
3478235

captcha