IQNA

Msikiti wa kwanza katika Uislamu kufanyiwa ukarabati

21:29 - April 08, 2022
Habari ID: 3475098
TEHRAN (IQNA)- Msikiti wa Quba katika mji wa Madina, ambao ni Msikiti wa kwanza katika Uislamu, unatazamiwa kufanyiwa ukarabati mkubwa na kuongeza ukubwa wake mara kumi zaidi.

Mradi huo unamaanisha kuwa mji wa Madina utashuhudia ustawi mkubwa zaidi katika historia hayo ambapo Msikiti wa Quba utapanuliwa kwa masafa ya mita mraba 50,000 na hivyo kuuwezesha kubeba waumini 60,000.

Mrithi wa Kiti cha Ufalme Mohammad bin Salman amesema mradi huo unalenga kuhudumia idadi kubwa ya waumini ambao hukosa nafasi. Aidha imedokezwa kuwa ukarabati wa msikiti huo utazingatia usanifu majengo wake wa kale.

Msikiti wa Quba ulikuwa msikiti wa kwanza katika Uislamu na uko umbali wa kilomita tano kutoka Msikiti wa Mtume SAW au Masjid Nabawi na ulijengwa mwaka wa kwanza Hijria Qamaria au 622 Miladia.

3478402

Kishikizo: msikiti wa quba madina
captcha