IQNA

Kasisi wa Kanisa la Koptik ahudhuria mashindano ya Qur'ani Misri

17:01 - April 24, 2022
Habari ID: 3475162
TEHRAN (IQNA)- Kasisi wa Kanisa la Koptik nchini Misri amehudhuria sherehe za kufunga mashindano ya kuhifadhi Qur'ani katika jimbo la Beheira nchini Misri.

Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar yaliwashirikisha wanafunzi 1,000 wa kike na kiume ambao walishindana kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

Akihutubu katika sherhe hiyo, Kasisi Yunus Adib amesema kushiriki kwake katika mashindano hayo kuna ujumbe wa ukarimu na udugu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Aidha amesema anauheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Vyombo vya habari vya Misri vimempongeza kasisi huyo na kuongeza kuwa amekuwa akiwapa futari Waislamu wasiojiweza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Misri ni nchi ya Kiislamu iliyo katika eneo la kaskazini mwa Afrika na idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa ni milioni 100. Wakristo wa dhehebu la Koptika wanakadiriwa kuwa takribani asilimia 10 ya watu wote katika nchi hiyo ya Kiarabu.

4051798

captcha