IQNA

Fikra za Imam Khomeini

Kiongozi Muadhamu: Imam Khomeini hakuwa wa jana tu bali ni wa leo na pia ni Imam wa kesho.

18:36 - June 04, 2022
Habari ID: 3475334
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshiriki katika Hauli ya mwaka wa 33 tokea alipoaga dunia muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema, "Imam Khomeini MA alikuwa roho ya Jamhuri ya Kiislamu'

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, Imam Khomeini, MA, alikuwa roho ya Jamhuri ya Kiislamu na kuongeza kuwa, Imam Khomeini MA alikuwa shakhsia wa kipekee kwa maana halisi ya neno hilo.

Ameongeza kuwa Imam hakuwa wa jana tu bali ni wa leo na pia ni Imam wa kesho.

Akihutubia umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria hauli hiyo ambayo baada ya kupita miaka miwili imeanza kufanyika tena kwa kuhudhuriwa na watu katika haram toharifu ya Kiongozi Mwanzilishi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei amelinganisha Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979 na Mapinduzi ya Ufaransa ya 1789 na halikadhalika Mapinduzi ya Shirikisho la Sovieti ya 1917 na kusema: “Mapinduzi hayo mawili ya Ufaransa na Sovieti yalipata ushindi kwa uungaji mkono wa wananchi lakini baada ya hapo wananchi hawakuzingatiwa na waliwekwa kando na hawakuweza kushirikishwa tena katika mapinduzi ambayo wao wenyewe walijitokeza mitani kuyanga mkono na kutoa maisha yao muhanga; matokeo ya hayo ni kuwa mapinduzi hayo yaliondoka katika mkondo asili wa wananchi.”

Mapinduzi ya wananchi

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kinyume cha mapinduzi hayo mawili, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipata ushindi kutokana na uungaji mkono wa wananchi na hata baada ya ushindi wananchi hawakutengwa. Amesema miezi mwili tu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kulifanyika kura ya maoni na wananchi wakaweza kuuchagua mfumo wautakao.

Aidha amesema mwaka moja baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, uchaguzi wa kwanza wa rais ulifanyika na miezi kadhaa baadaye, uchaguzi wa kwanza wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu au bunge ulifanyika na hadi kufikia sasa karibu chaguzi 50 zimefanyika nchini tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na wananchi wamekuwa wakishiriki kwa wingi katika chaguzi hizo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, katika Jamhuri ya Kiislamu, nafasi ya wananchi ni yenye umuhimu sana na maadui hawataweza kuwachonganisha wananchi na Mfumo wa Kiislamu.

Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, ni jambo la yakini kwamba, leo mapenzi ya watu kwa dini na mapinduzi ni makubwa zaidi kuliko mwanzoni mwa mapinduzi; na akalibainisha hilo kwa kutoa mifano kadhaa ya jinsi wananchi hao walivyojitokeza kwa wingi mno katika kuuenzi muqawama na wanazuoni wa kidini.

Kusindikzwa Shahidi Soleimani

Amesema, kusindikizwa na mamilioni ya watu mwili uliokatika vipande vipande wa Shahidi Soleimani na kuenziwa mno mwanamapinduzi, mpambanaji na mujahidina huyo; na kusindikizwa na watu waliojawa na hisia kubwa za mapenzi Maraajii na Mafaqihi watajika walioaga dunia kama Ayatullah Safi Golpaigani na Ayatullah Bahjat kulikuwa kwa namna isiyoweza kulinganishwa na alivyoenziwa shakhsia yeyote wa kisiasa na wa usaniii nchini; na hilo linaonyesha itikadi na imani ya watu kwa wanazuoni, dini jihadi na muqawama. 

Katika sehemu nyingie ya hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezifanyia uchambuzi sababu za maadui wa Iran kupanga mahesabu yao kimakosa kila mara, kwa kuashiria nafasi ya washaurii wao kadhaa ambao ni Wairani wasaliti, katika upangaji wa mahesabu na mikakati hiyo na akasema: washauri hawa mahaini hawaisaliti nchi yao pekee, bali wanawasaliti Wamarekani pia, kwa sababu, kwa kuwapatia ushauri huo potofu wanawafanya washindwe.

Uadui na uharamia baharini

Halikadhalika, Ayatullah Khamenei amesema, moja ya sababu za uadui unaofanywa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ni Imam Khomeini (MA) alivyojipambanua na kujitenganisha na Wamagharibi na akalifafanua hilo kwa kusema: kuihami Palestina na kulipatia taifa la Palestina ubalozi wa utawala ghasibu wa Kizayuni na kuuokosoa waziwazi uzandiki na jinai za nchi za Ulaya na Marekani ni mifano muhimu ya jinsi Imam Khomeini alivyopambanua na kutenganisha ustaarabu, fikra na mfumo wa Kiislamu na ustaarabu na fikra ya Kimagharibi.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia pia uharamia wa baharini ambao serikali ya Ugiriki imeifanyia Iran na akasema, siku kadhaa nyuma na kwa amri ya Marekani, Ugiriki iliiba mafuta ya Iran, lakini wakati askari mashujaa waliojitolea mhanga wa Jamhuri ya Kiislamu walipoikamata meli ya adui, zilifanywa propaganda chungu nzima za kuituhumu Iran kuhusika na wizi, ilhali ni wao walioiba mafuta yetu; na kurejesha mali iiliyoibiwia si wizi.

3479169

captcha