IQNA

Ibada ya Hija

Saudia yaondoa masharti ya corona huku msimu wa Hija ukianza

23:35 - June 14, 2022
Habari ID: 3475377
TEHRAN (IQNA)- Mamlaka ya Saudia ilitangaza Jumatatu kuondolewa kwa amri ya barakoa katika maeneo ya ndani huku Waislamu kutoka kote ulimwenguni wakiwasili kuanza nchhini humo kuanza ibada ya Hija.

Hatua hiyo inajiri huku ufalme huo ukijiandaa kuwakaribisha takriban mahujaji 850,000 kutoka nje ya nchi kushiriki katika ibada ya kila mwaka ya Hija.

Kundi la kwanza la Mahujaji wa kigeni tangu kuanza kwa janga la COVID-19 au corona lilianza kuwasili kutoka Indonesia mapema mwezi huu.

Kwa mujibu wa sheria zilizowekwa barakoa  bado zinahitajika katika maeneo matakatifu zaidi ya Kiislamu ya Makka na Madina, ambapo mahujaji hukusanyika kwa ibada. Aidha waandaaji wa hafla na  sherehe kote Saudia wanahiari ya kuwataka washirika kuvaa barakoa.

Ufalme huo pia ulitupilia mbali sheria inayohitaji uthibitisho wa chanjo kwenye programu ya simu ambayo ilihitajika kuingia sehemu fulani, kuhudhuria hafla na kupanda ndege.

Uvaaji wa barakoa na utumiaji wa programu umetekelezwa kwa kiasi kidogo katika miezi ya hivi karibuni.

Janga la COVID-19 limetatiza sana ibada ya Hija, ambayo kwa kawaida huingizia Saudia pato la takribani dola bilioni 12 kila mwaka.

Kwa takriban miaka miwili, Saudi Arabia ilikuwa miongoni mwa nchi zilizoweka vikwazo vikali zaidi duniani katika juhudi zake za kupunguza kuenea kwa virusi vya corona.

Sheria hizo zilijumuisha kupiga marufuku raia wa Saudia kuondoka nchini, kuwazuia wasafiri kutoka nchi nyingi kuingia Saudi Arabia, kuhitaji uthibitisho wa chanjo ya kuingia kwenye maduka makubwa na maeneo mengine ya ndani na pia waliohiji katika mika hiyo miwili walikuwa ni Waislamu wanaoishi ndani ya Saudia tena kwa idadi ndoge sana.

Saudia sasa imelegeza sheria zake huku ikitumai kuwavutia watalii chini ya mpango mpya wa kukuza uchumi.

Wakati huo huo, katika nchi jirani ya Umoja Falme za Kiarabu, serikali inasisitiza umuhimu wa kuvaa barakoa katika mijimuiko ya ndani ya majengo au kumbi huku kukiwa na ongezeko la asilimia 100 la kesi mpya za corona chini ya wiki moja. Nchi hiyo yenye  wakaazi milioni 9 ina karibu watu 1,300 waliothibitishwa kuambukizwa upya corona  licha ya viwango vya juu vya chanjo.

Mtu yeyote atakayepatikana akikiuka sheria za kuvaa barakoa maeneo ya ndani nchini UAE atatozwa faini ya dirham 3,000, au takriban US $815.

3479297

captcha