IQNA

Ugaidi Marekani

Mmarekani ashtakiwa kwa kujaribu kuanzisha tawi magaidi wa Daesh jimboni New Mexico

12:02 - August 28, 2022
Habari ID: 3475692
TEHRAN (IQNA) – Mmarekani mmoja katika jimbo la New Mexico nchini Marekani ameshtakiwa kwa kujaribu kuanzisha kituo cha mafunzo kwa watu wanaotaka kujiunga na kundi la kigaidi la Daesh (ISIL au ISIS).

Wizara ya Sheria ya Marekani ilitangaza hayo Ijumaa.

Mnamo Agosti 23 maafisa wa mahakama walimshtaki Herman Leyvoune Wilson, 45, wa Albuquerque, kwa kujaribu kutoa msaada wa nyenzo kwa kundi la  kigaidi la Daesh kwa kuanzisha kituo cha Daesh huko New Mexico.

Kituo hicho kililenga kufundisha itikadi za Daesh, kutoa mafunzo ya "karate," na kuwa kambi kwa watu binafsi wanaojiandaa kupigana kwa niaba ya kundi hilo nchini Marekani na nje ya nchi, ilisema taarifa hiyo.

Wilson, anayejulikana pia kama Bilal Mu'Min Abdullah, alisaidia kuendesha jukwaa la mtandaoni ambalo lilipigia debe uandikishaji wa wanaotaka kujiunga na Daesh na kujadili mashambulizi nchini Marekani na nje ya nchi, ilisema taarifa hiyo.

Wanaume wawili waliohukumiwa mwezi Julai kwa kutoa msaada kwa Daesh walisema Wilson aliwaleta kwenye kundi hilo, waendesha mashtaka walisema.

Kristopher Matthews, 36, wa South Carolina na Jaylyn Molina, 24, wa Texas walisema Wilson aliwabadilishia na kuwafanya wafuate "itikadi za ISIS," taarifa hiyo ilisema.

Kwingineko, Awais Chudhary, 22, wa New York siku ya Ijumaa alikiri hatia ya kupanga shambulio la kisu katika mtaa wa Queens kwa niaba ya Daesh, Idara ya Sheria ilisema katika taarifa.

Daesh ni kundi la magaidi wakufurishaji na weledi wa mambo wanasema kundi hilo lilianzishwa kwa njia ya moja kwa moja  au isiyo ya moja kwa moja na Marekani kwa ushirikiano na waitifake wake hasa utawala haramu wa Israel kwa lengo la kueneza ghasia katika eneo la Asia Magharibi.

3480227

 

captcha