IQNA

Mkuu wa ICRO katika mkutano na Askofu wa Armenia

Wakisristo na Waislamu wakuze maisha kidini

22:11 - August 30, 2022
Habari ID: 3475707
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu Iran (ICRO) anasema moja ya majukumu ya pamoja ya Uislamu na Ukristo ni kukuza nafasi ya dini katika maisha ya watu binafsi.

"Moja ya dhamira zetu za leo ni kujitahidi kuwa na maisha sahihi yanayotegemea dini," mkuu wa ICRO Hujjatul Islam Mohammad Mehdi Imanipour alisema Jumatatu katika mkutano na Sebouh Sarkissian, Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Armenia ya Tehran.

Dini zote za Ibrahimu zina kanuni za pamoja na msimamo huu wa pamoja unaweza kuwa msaada mzuri wa kupanua uhusiano, alisema mwanazuoni huyo wa  Iran.

Akizungumzia faida za mazungumzo ya dini mbalimbali na msisitizo wa ICRO wa kuendeleleza mazungumzo hayo, Imanipour amesema kuwa mazungumzo hayo yanatafuta amani na kuishi pamoja kwa amani.

Wasomi wa Uislamu na Ukristo wanaweza kuchukua jukumu muhimu katika kupunguza uchungu wa wanadamu wa leo, aliongez.

Pia alitumai kuwa duru ya tisa ya mazungumzo ya kidini na kanisa la Armenia inaweza kufanywa hivi karibuni.

Fira ya zama za Renaissance au mwamako barani  ilikuwa udanganyifu ambao baadhi ya serikali kuu za ulimwengu zilianzisha ili kuondoa dini ili kukabiliana na serikali ya kidini, alisema, na kuongeza, "Hatuwezi kukataa makosa yaliyofanywa na Kanisa lakini makosa hayo yalikuwa ni sehemu ya visingizio vya kuondoa dini kutoka kwa jamii."

Njama za kina sasa zinaendelea kudhuru maisha ya kidini, alisema.

Kwa upande wake, Askofu Sarkissian aligusia uhusiano wa miaka 23 kati ya Kanisa la Armenia na ICRO, akibainisha kuwa alilifahamu shirika hilo wakati hayati Ayatollah Taskhiri alipokuwa mkuu wake. "Ninahisi niko nyumbani hapa."

Aidha alijuta kwamba wanadamu wa leo wanajitenga na dini.

Askofu huyo pia alitumai kuwa duru inayofuata ya mazungumzo ya dini mbalimbali inaweza kufanyika mapema mwaka ujao.

4081796

captcha