IQNA

Waislamu Burkina Faso

Vikao vya Qur'ani Tukufu nchini Burkina Faso

15:41 - December 17, 2022
Habari ID: 3476261
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha uenezi cha kimataifa chenye mfungamano na Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) mjini Karbala, Ira kimeandaa duru za Qur'ani na programu za elimu kwa wanafunzi wa shule na vyuo vikuu nchini Burkina Faso.

Tawi la kituo hicho katika nchi ya Afrika limeshirikiana katika kufanya programu hizo, ambazo zimehudhuriwa na makumi ya wanafunzi.

Taasisi ya Warith al-Anbiya katika mji wa Bobo-Dioulasso imekuwa ikiandaa vikao hivyo vya mafunzo ya Qur'an Tukufu, amesema Ali Aboud al-Taei, Mkuu wa Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS) inayosimamia ya shughuli za Qur'ani barani Afrika.

Washiriki wa vikao hivyo ambavyo hufanyika Jumamosi na Jumatano hupata mafunzo ya usomaji wa Qur'ani na matamshi sahihi ya aya za Qur'ani Tukufu, aliongeza.

Al-Taei aliendelea kusema kwamba programu hizo zimepangwa kama sehemu ya mkakati wa Idara ya Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Hussein (AS)  wa kukuza utamaduni wa Qur'ani.

Burkina Faso ni nchi isiyo na bandari katika Afrika Magharibi, imezungukwa na nchi sita: Mali kwa upande wa kaskazini; Niger upande wa mashariki; Benin kuelekea kusini mashariki; Togo na Ghana upande wa kusini; na Ivory Coast upande wa kusini magharibi.

Uislamu nchini Burkina Faso una historia ndefu na tofauti. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2010, takriban asilimia 62 ya wakazi wa nchi hiyo ni Waislamu.

Quranic Circles, Educational Programs for Students Being Held in Burkina Faso

Quranic Circles, Educational Programs for Students Being Held in Burkina Faso

Quranic Circles, Educational Programs for Students Being Held in Burkina Faso

Quranic Circles, Educational Programs for Students Being Held in Burkina Faso

4107443

captcha