IQNA

Umoja wa Kiislamu

Maulamaa wa Kisunni kutoka Iran wakutana na Mufti wa Tanzania

12:54 - December 29, 2022
Habari ID: 3476324
TEHRAN (IQNA) - Ujumbe wa Maulamaa wa Kisunni wa Iran umekutana na kufanya mazungumzo na Mufti wa Tanzania Jumanne.

Ujumbe huo kutoka Mkoa wa Golestan kusini mwa Iran, ulikutana na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry ikiwa ni sehemu ya programu zao nchini Tanzania.

Sheikh Salaheddin, mwanzilishi wa Chuo cha Kiislamu cha Chenarli katika mkoa Golestan, amesema lengo la ziara hiyo nchini Tanzania ni  kukutana na "ndugu wa kidini", kufahamiana na tamaduni na mila za watu Tanzania, na kutembelea vyuo vya Kiislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Katika kikao hicho Sheikh Salaheddin pia ametoa maelezo mafupi kuhusu Chuo cha Kiislamu cha Chenarli. Halikadhalika akizungumza katika mkutano huo, Sheikh Esmail Ghadiri, Imamu wa Sala ya Ijumaa ya katika mji wa Chenarli, alisema kuwa Waislamu wa madhehebu za Shia na Sunni wanaishi pamoja kwa maelewano mazuri kote Iran.

Naye mkurugenzi wa Chuo cha Kiislamu cha Chenarli Sheikh Issam Uddin alisema misikiti ya Waislamu wa Kisunni imepanuka tangu kuanza kwa Mapinduzi ya Kiislamu mwaka 1979 na kuongeza kuwa hivi sasa idadi ya misikiti ya Kisunni ni zaidi ya misikiti ya Kishia  katika mkoa wa Golestan,

Kwa upande wake, mufti wa Tanzania alifurahia ziara ya ujumbe wa Iran, na kuelezea mikutano hiyo kuwa ya thamani kubwa.

Akizungumzia haja ya kustawisha umoja katika ulimwengu wa Kiislamu, Sheikh Zubeiry alisema ataitembelea Iran katika kipindi cha miezi miwili ijayo ili kujifahamisha kuhusu mafanikio ya kisayansi na kiutamaduni ya wanazuoni wa Kiislamu nchini Iran.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa tawi la Tanzania, Hujjatul Islam Ali Taghavi, pia alishiriki katika mkutano huo.

Delegation of Iranian Sunni Clerics Meet Tanzania’s Mufti

3481862

captcha