IQNA

Waislamu Afghanistan

Ayatullah Sistani ahimiza uungwaji mkono kwa Afghanistan

17:08 - January 04, 2023
Habari ID: 3476357
TEHRAN (IQNA) – Kiongozi mkuu wa Waislamu wa Kishia nchini Iraq Ayatullah Seyed Ali al-Sistani amehimiza jumuiya ya kimataifa na Waislamu kote ulimwenguni kuunga mkono watu "wanaoteseka" nchini Afghanistan.

Aliyasema hayo katika mkutano wa Jumanne katika ofisi yake yenye makao yake makuu mjini Najaf akiwa na ujumbe i wa Baraza la Ulamaa wa Kishia la Afghanistan.

Akirejelea uhalifu na ukandamizaji ambao watu wa Afghanistan, hususan wanawake, wanakabiliana nao, alielezea masikitiko yake kwa yale ambayo watu hao wamepitia katika miongo michache iliyopita.

"Waislamu na jumuiya ya kimataifa hawapaswi kuwaacha watu wa Afghanistan peke yao chini ya mazingira kama hayo na hawapaswi kuacha jitihada zozote za kupunguza mateso yao," Ayatullah Sistani alisisitiza.

Aidha ameashiria umuhimu wa kudumisha umoja wa kitaifa na kuishi pamoja kwa amani nchini Afghanistan.

"Mtu anapaswa kuepuka vurugu katika kushughulika na watawala wa sasa wa Afghanistan," alibainisha.

Alitoa wito kwa baraza la Shia kufanya "chochote wanachoweza" ili kupata haki za taifa la Afghanistan.

Wajumbe wa baraza hilo kwa upande wao waliwafahamisha Ayatullah Sistani ambaye pia ni Marjaa Taqlid wa Mashia wengi duniani kuhusu hali ya Afghanistan na hatua zinazotekelezwa na baraza hilo.

4112113

captcha