IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu Afrika Kusini yafanyika Pretoria

12:19 - January 19, 2023
Habari ID: 3476429
TEHRAN (IQNA) – Toleo la 13 la mashindano ya kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Afrika Kusini yalifanyika katika mji mkuu, Pretoria.

Baraza la Taifa la Qur'ani la Afrika Kusini (SANQC) liliandaa hafla hiyo iliyohudhuriwa na wahifadhi wa Qur'ani kutoka kote katika nchi hiyo.

Mashindano hayo yalifanyika katika Msikiti wa Nour wa Pretoria ambapo Imamu na mhubiri wa Msikiti Mkuu wa Makka, Maher bin Hamad bin Muhammad bin al-Mu’aiqly al-Balawi, alihudhuria sherehe za kufunga, ambapo washindi wakuu walitunukiwa.

Akihutubu katika hafla hiyo, al-Balawi alipongeza shindano hilo na kusema matukio kama haya yanasaidia kuwahimiza wavulana na wasichana wadogo kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu.

SANQC ni shirika la Kiislamu nchini Afrika Kusini, lililoanzishwa kwa madhumuni ya kutumikia Qur'ani Tukufu.

"Katika juhudi zetu za kufikia lengo hili, mradi wetu mkuu ni Mashindano ya kila mwaka ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu nchini Afrika Kusini. Kupitia mashindano hayo tunataka kuhimiza Jumuiya ya Kiislamu ya Afrika Kusini kuhifadhi Qur'ani Tukufu, kufanya vyema katika usomaji wake sahihi na kukuza masomo ya Sayansi ya Qur'ani," kwa mujibu wa tovuti ya baraza hilo.

 4115503

captcha