IQNA

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran

Zilzala Uturuki na Syria ni janga kubwa la binadamu, jamii ya kimataifa imeshindw katika mtihani huu

19:41 - February 17, 2023
Habari ID: 3476573
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amekosoa mienendo ya nchi za Magharibi kuhusiana na tetemeko la ardhi nchini Syria.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Mohammad Javad Haj Ali Akbari amesema katika hutuba za Sala ya Ijumaa, kuwa mitetemekomikubwa ya ardhi iliyotokea Uturuki na Syria lilikuwa janga kubwa la binadamu, na jamii ya kimataifa imeshindwa na kufeli katika mtihani huo.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari alifafanua kuwa Marekani na Ulaya zimekumbwa na mporomoko wa kimaadili na zimedhihirisha dhati zao chafu katika zilzala nchini  Syria.

Imamu wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuma timu za waokoaji na shehena za misaada ya kibinadamu kwa ajili ya kuisaidia Uturuki na Syria, na ameeleza matumaini yake kuwa, mashaka ya mataifa hayo mawili azizi ya Uturuki na Syria yatapungua kwa juhudi za mataifa ya kanda ya Magharibi mwa Asia na wananchi wa Iran.

Nchi za Magharibi zinalaumiwa kwa kuwabagua na kuwatelekeza watu waliokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi nchini Syria na kuingiza masuala ya siasa katika zoezi la kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathiriwa na janga hilo.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Haj Ali Akbari pia ameashiria ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini China na kusema kuwa safari hii ina taathira za kitaifa kwa nchi zote mbili na pia athari za kikanda na kimataifa ambazo baadhi yake zimeanza kuonekana na mengine yatatokea katika siku zijazo.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia imetuma shehena kadhaa za misaada katika nchi za Syria na Uturuki kuwasaidia walioathirika na mitetemeko ya ardhi. Jeshi la Iran pia limejenga hospitali ya muda ya vitanda 50 katika eneo la Adiyaman la Uturuki inayowahudumia wagonjwa wasipoungua 100 kwa siku.

Ikumbukwe kuwa Februari sita mitetemeko miwili mikubwa ya ardhi yenye ukubwa wa 7.8 na 7.5 kwa kipimo cha Rishta iliyakumba maeneo ya kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria. Hadi sasa karibu watu elfu 45 wameripotiwa kuaga dunia katika janga hilo la kimaumbile. 

4122700

captcha