IQNA

Mwanasiasa Anayepinga Uislamu Amepigwa Marufuku kwenye Tamasha la Kisiasa la Denmark

14:15 - June 17, 2023
Habari ID: 3477151
Rasmus Paludan, mwanasiasa wa Denmark mwenye siasa kali za chuki dhidi ya Uislamu alipigwa marufuku kushiriki katika tamasha la kisiasa la Folkemodet katika kisiwa cha Bornholm.

Paludan anajulikana kwa maandamano yake yenye utata ya kuchoma Qurani Tukufu  nchini Denmark na Sweden. Mamlaka ya polisi wa eneo hilo siku ya  Jumanne ilipiga marufuku ya kuwepo kwa Paludan kuzunguka eneo la tamasha ndani na karibu na kijiji cha Allinge kuanzia Mwezi  Juni  Tarehe 14 asubuhi hadi adhuhuri ya Mwezi  Juni Tarehe  18 kwa misingi kwamba uwepo wake ungewakilisha hatari kwake mwenyewe na washiriki wengine.

Paludan alichoma nakala za kitabu kitukufu  cha Waislamu, Qurani Tukufu , karibu na msikiti na nje ya majengo ya Ubalozi wa Uturuki mjini Copenhagen mapema mwaka huu,  Kitendo hicho kilivutia shutuma kutoka kote ulimwenguni.

Akijibu matukio hayo, Denmark ilisema na kusisitiza kuwa haitaharibu  uhusiano wake mzuri na Uturuki.

Kazi yetu sasa ni kuzungumza na Uturuki kuhusu jinsi hali ilivyo nchini Denmark na demokrasia yetu wazi, na kwamba kuna tofauti kati ya Denmark kama nchi  na watu wetu, na kisha kuhusu watu binafsi ambao wana maoni tofauti,  Waziri wa Mambo ya Nje Lars Lokke Rasmussen alisema;

Kuchafuliwa kwa Qurani Tukufu  kulizusha maandamano makubwa katika ulimwengu wa Kiislamu, huku Uturuki ikilaani vikali ruhusa iliyotolewa na mamlaka kwa kitendo hicho cha uchochezi ambacho ilisema ni uhalifu wa chuki dhidi ya Uislamu.

 

3483945

 

captcha