Mji mtakatifu wa Makaa unaandaa toleo la 43 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Mfalme Abdulaziz katika kuhifadhi, kusoma na kutafsiri.
Mashindano hayo yanayoanza leo yatafanyika kwa siku 11 kwenye Msikiti Mkuu wa Makka (Al Masjid Al Haram) eneo takatifu zaidi katika Uislamu.
Hafla hiyo imeandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia, na kupewa jina la mwanzilishi wa marehemu wa Saudi Arabia, Mfalme Abdulaziz.
Mashindano ya mwaka huu yamevutia washiriki 166 kutoka nchi 117, kwa mujibu wa msimamizi mkuu wa wizara hiyo Abdelatif Al Alsheikh.
Aliongeza kuwa jumla ya thamani ya zawadi hizo imeongezeka na kufikia zaidi ya dola milioni moja mwaka huu, huku mshindi bora akipata dola 133,000. Wizara imekuwa ikifanya mashindano hayo ya kila mwaka tangu 1979.
3484916