IQNA

Jinai za Israel

Kanisa Palestina laweka magofu badala ya Mti wa Krismasi, lasema hakuna cha kusherehekea

17:05 - December 05, 2023
Habari ID: 3477989
BEIT LAHM (IQNA)- Kanisa moja la Palestina limeamua kuweka kunyesha magofu ya nyumba zilizobomolewa badala ya Mti wa Krismasi kama ilivyo ad ana kusema kuwa hakuna cha kusherehekea wakati huu utawala haramu wa Israel unapendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Krismasi huko Bethlehemu katika mji wa kihistoria Beit Lahm (Bethlehem) katika eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi linaokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel limesisitiza kuwa mwaka huu hakutakuwa na sherehe za krismasi kama ilivyozoleka.

Kasisi Munzir Ishak wa kanisa hilo amesema: Wakati mauaji ya halaiki yanafanywa dhidi ya watu wetu huko Ghaza, hatuwezi kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo (Nabii Isa Masih) mwaka huu kwa njia yoyote. Hatujisikii kusherehekea."

Ingawa mitaa katika ulimwengu wa Kikristo imepambwa wakati huu wa kukaribia Krismasi, makanisa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu yanajiepusha  na sherehe za kupita kiasi, huku yakijikita zaidi katika ibada.

Kwa hivyo, badala ya kupamba kanisa kwa mti wa Krismasi mwaka huu, kanisa hilo lilichagua mapambo yaliyotengenezwa kutoka kwa magofu kuashiria uharibifu unaotekelezwa na Israel katika vita vyake vya maangamizi ya umati dhidi ya Wapalestina huko Ghaza.

Kasisi Ishak alisema kutumia magofu  badala ya mapambo ya Krismasi kanisani ni ujumbe kwa waumini wa kanisa hilo na pia  kwa ulimwengu.

Kasisi huyo alisema: "jumbe wetu kwetu sisi wenyewe ni huu: Mungu yu pamoja nasi katika maumivu haya na pili, tulitaka kuyaambia makanisa duniani kote kwamba, kwa bahati mbaya, Krismasi huko Palestina ni kama hii.' Iwe ni Wakristo au Waislamu, hii ndiyo hali tunayopitia Palestina. Tunakabiliana na vita vya mauaji ya halaiki vinavyolenga Wapalestina wote. Kwa bahati mbaya, tunapofikiria kuzaliwa kwa Nabii Isa, tunafikiria watoto wachanga waliouawa kikatili huko Gaza."

Makasisi wa Kikristo  Palestina wanasisitiza kwamba mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza "yameua roho ya Krismasi."

Wakristo kutoka sehemu mbalimbali za dunia hutembelea mji wa Beit Lahm mwishoni mwa mwezi wa Disemba kila mwaka kusherehekea Krismasi, wakiamini kuwa ndiko alikozaliwa Nabii Isa-Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake.-

Tangu kuanza kwa vita vya Israel kwenye Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba, jeshi la Israel limeharibu kabisa misikiti 88, pamoja na kuharibu kwa sehemu mingine 174. Vikosi vya Israel pia vimlenga makanisa matatu, kulingana na ofisi ya serikali ya vyombo vya habari huko Gaza.

3486300

Habari zinazohusiana
captcha