IQNA

Mgogor

Yemen yasema hujuma ya Marekani na Uingereza haitazima uungaji mkono taifa la Palestina

18:55 - January 12, 2024
Habari ID: 3478186
IQNA-Msemaji wa majeshi ya Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Sarii amesema kuwa, mashambulizi ya kiuadui ya Marekani na Uingereza hayatobadilisha msimamo wa Yemen wa kuliunga mkono taifa la Palestina ikiwemo Gaza na kwamba uadui huo uliofanyika mapema leo Ijumaa dhidi ya Yemen hautoachwa vivi hivi bila ya majibu na kuadhibiwa madola hayo ya kibeberu.

Amesema kuwa, madola ya kibeberu ya Marekani na Uingereza zimeshambulia mashambulizi 73 dhidi ya maeneo tofauti ukiwemo mji mkuu San'a na mikoa ya Al Hhudaida, Tais, Hajjah na Sa'ada na kusababisha kuuawa shahidi askari watano wa Yemen na kujeruhiwa wengine sita.

Amesema, Marekani na Uingereza ndizo zinazobeba dhima yote ya kitakachofuatia baada ya mashambulizi yao hayo ya kijinai na kwamba hayawezi kuachwa hivi hivi bila ya kuadhibiwa Marekani na Uingereza. 

Kabla ya hapo pia, Mkuu wa Timu ya Mazungumzo ya Yemen alikuwa tayari amesema kuwa, uadui wa Marekani na Uingereza dhidi ya nchi hiyo hautolizuia taifa hilo kusimama bega kwa bega na ndugu zao Wapalestina wakiwemo wa Ukanda wa Ghaza.

Mohammad Abdul Salaam amesema hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X na kusisitiza kuwa, uadui wa wazi wa Marekani na Uingereza dhidi ya taifa la Yemen umefanyika ili kuunga mkono utawala wa Kizayuni na kujaribu kukabiliana na operesheni za Yemen za kuzuia meli zisielekee kwa utawala wa Kizayuni wa Israel, lakini taifa la Yemen litaendelea kuwa pamoja na wananchi wa Palestina na kwamba mashambulizi hayo hayatolifanya taifa hilo shujaa kulegeza msimamo wake.

Ameongeza kuwa, Marekani na Uingereza zimefanya kosa la kipumbavu kwa hatua yao ya kuanzisha mashambulio dhidi ya Yemen kwa kudhani kuwa zinaweza kulizuia taifa hilo kuwasaidia Wapalestina na kusisitiza kuwa, Yemen itaendelea na msimamo wake huo wa kidini na kibinadamu na haitotetereshwa na mashambulizi kama hayo ya maadui.

Ameongeza kuwa, Yemen haikuwa inahatarisha usalama wowote wa baharini isipokuwa iliamua kuzuia meli za Israel tu kutumia maji ya Yemen kuelekea kwa utawala huo, lakini meli na vyombo vyote vingine vilikuwa vinapita kwa uhuru na usalama kamili kwenye Bahari ya Sham na Lango Bahari la Bab al Mandab hivyo hakukuwa na sababu yoyote ya kufanyika mashambulizi hayo ya kiuadui ya Marekani na Uingereza isipokuwa tu kwa ajili ya kuunga mkono jinai za Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

Tayari jeshi la Yemen limetangaza kushambulia manuwari za Marekani na Uingereza kujibu jinai hizo za mapema leo Ijumaa na limeahidi kutoa mashambulizi makali dhidi ya maadui hao kwa namna ambayo hawakuitarajia.

Vile vile limesema kuwa, litaendelea kuzuia meli zote za Israel na zile zinaoelekea kwa utawala wa Kizayuni kupita kwenye maji ya Yemen hadi Israel itakapokomesha jinai zake Ghaza.

4193460

captcha