IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Qari wa Iran kuhudhuria kikao cha kusoma Qur'ani Tukufu Sydney

16:19 - January 23, 2024
Habari ID: 3478239
IQNA – Kikao cha usomaji wa Qur'ani Tukufu imepangwa kufanyika Sydney, Australia, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ali (AS).

Chuo cha Samen Al-Aeme Imam Reza Quran Academy mjini Sydney kitaandaa hafla hiyo baada ya swala ya Maghrib na Isha Ijumaa hii.

Msomaji mashuhuri wa Qur'ani Tukufu wa Iran Hadi Esfandani atakuwa qari mgeni maalum katika programu hiyo.

Mustafa Ashrafi, mwanaharakati wa Qur'ani wa Iran nchini Australia, pia atashiriki katika duru ya Qur'ani.

Chuo cha Samen Al-Aeme Imam Reza Quran Academy ni taasisi ambayo hupanga programu mbalimbali za Qur'ani na kidini kwa ajili ya Waislamu mjini Sydney na kwingineko nchini Australia.

Ni pamoja na mashindano ya Qur'ani ambayo yanapokelewa vyema na Waislamu wa nchi hiyo.

Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengineo husherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imam Ali (AS) katika siku ya 13 ya mwezi wa mwandamo wa Rajab, ambayo mwaka huu inaadhimishwa Alhamisi, Januari 25.

Imam Ali (AS) alikuwa mkwe na binamu yake Mtume Muhammad (SAW) na pia Imam wa kwanza katika Uislamu wa Shia.

Imam anaheshimika kwa ujasiri wake, elimu, imani, uaminifu, utiifu usiopinda kwa Uislamu, uaminifu mkubwa kwa Mtume Muhammad (SAW), kuwatendea sawa Waislamu wote na ukarimu wa kuwasamehe maadui zake walioshindwa.

4195402

captcha