IQNA

Mapinduzi ya Kiislamu

Raisi: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaongoza mapambano dhidi ya ugaidi na kutetea haki za binadamu duniani

19:16 - February 11, 2024
Habari ID: 3478335
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi amesema: Jamhuri ya Kiislamu inaongoza mapambano dhidi ya ugaidi na kutetea haki za binadamu.

Raisi ameyasema hayo leo katika umati mkubwa wa waandamanaji waliokusanyika mjini Tehran kuadhimisha mwaka wa 45 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, siku ambayo ni maarufu kama 22 Bahman. Ameashiria jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza na misaada na himaya ya Marekani kwa utawala huo, akitilia mkazo udharura wa kusitishwa haraka mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina. Amesema: Licha ya njama zisizosita za Wamagharibi, Iran inaendelea kuiunga mkono Palestina na fikra za Mapinduzi ya Kiislamu, na baada ya miaka 45 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, imethibitika kuwa haki iko upande wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Imam Ruhullah Khomeini ambaye alisema Palestina ndiyo kadhia nambari moja ya Umma wa Kiislamu na kwamba Quds lazima ikombolewe.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njia ya kuuangamiza utawala wa Kizayuni na kukomesha jinai zake ni kukata uhusiano na milingano yote ya kiuchumi na utawala huo ghasibu. Amasisitiza kuwa: Pendekezo la Iran ni kufukuzwa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Umoja wa Mataifa na kuhoji kwamba: Utawala ambao umekiuka matamko, maazimio na sheria 400 za mashirika ya kimataifa unawezaje kuzingatia maagizo na maazimio ya Umoja wa Mataifa?
​Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Rais Ebrahim Raisi amesema kwamba, uhuru wa watu unalindwa na kudhaminiwa ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa: Wanaodai kutetea demokrasia hawaheshimu kura za Wapalestina na Wayemeni na hata kura za mataifa yao wenyewe. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, adui ameanzisha vita vya kijeshi, kiuchumi, vyombo vya habari, kisaikolojia na vita mseto vya karibuni kwa shabaha ya kusimamisha harakati ya maendeleo ya taifa la Iran. Amesema fikra ya Mapinduzi ya Kiislamu inatoa ujumbe wa ukombozi na uhuru wa mataifa na ujumbe wa mapambano na kusimama kidete dhidi ya maadui.

Sayyid Ebrahim Raisi amesema kwamba, maendeleo ya Iran ya Kiislamu yamepatikana katika kivuli cha kumwamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu na kujiamini, na katika muktadha huu Iran imeshika nafasi ya 15 ya maendeleo ya kisayansi duniani.

Ameongeza kuwa: Kwa baraka za Mapinduzi ya Kiislamu na juhudi za vijana, Iran sasa ni miongoni mwa vinara wa dunia katika nyuga za tiba, bioteknolojia na nanoteknolojia.

4199013

Habari zinazohusiana
captcha