IQNA

Umrah

Saudia yaboreseha huduma za Mahujaji wa Umrah mwezi wa Ramadhani

15:31 - March 13, 2024
Habari ID: 3478501
IQNA - Matayarisho yote yamefanywa ili kuhakikisha mchakato mzuri na uliorahisishwa wa taratibu za kuwasili na kuondoka kwa wanaofika Saudia kwa ajili ya Hija ndogo ya Umrah wakati wa Mwezi wa Ramadhani.

Kurugenzi Kuu ya Pasipoti ya Saudia imetangaza utayari wake wa kuwapokea Mahujaji wa Umrah wanaofika katika vituo vya kuvuka mpaka vya Ufalme wa Saudia wakati wa mwezi mtukufu, Shirika la Habari la Saudia liliripoti Jumatatu.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa afisi zote za pasipoti katika vituo vya kuvuka mpaka zimewekewa wafanyakazi na vifaa vya kisasa ikiwa ni pamoja na vifaa vya kutafsiri vituo ziada vya kuchunguza pasipoti.

Kurugenzi hiyo pia ilisisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni na maelekezo kuanzia kufika kufanya Umrah hadi kuondoka.

Wakati huo huo, Shirika la Reli la Saudi Arabia lilitangaza utayarifu wa Reli ya Kasi ya Haramain kuwahudumua waumini na wageni kwenye Misikiti Miwili Mitakatifu wakati wa Ramadhani.

Mipango yote ya uendeshaji imekamilika, na reli ya mwendo kasi iko tayari kwa wageni katika maeneo mbalimbali kati ya Makka na Madina.

Shirika hilo limesema kuwa kutakuwa na zaidi ya safari 2,700 za treni  katika Ramadhani, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9 kutoka mwaka jana. Upatikanaji wa viti pia uliongezeka kwa asilimia 26, na hivyo kupindukua milioni 1.3.

Kwa kuzingatia mipango ya mwaka jana, Shirika la Reli la Saudi Arabia bado limejitolea kufanya kazi na washirika wake ili kuhakikisha safari bora kwa waumini wote wakiwamo waliofika nchini humokwa ajili ya Umrah.

Ratiba za treni zitarekebishwa ili kuendana na nyakati za Sala  Makka na Madina.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: ramadhani umrah
captcha