IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya wenye vipaji maalumu

10:44 - April 22, 2024
Habari ID: 3478716
IQNA - Misri inaandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa wenye vipaji maalumu lengo likiwa ni  kukuza utamaduni wa Kiislamu.

Mashindano hayo yalianza katika sherehe huko Sharm El Sheikh, mji ulio kwenye ncha ya kusini ya Rasi ya Sinai, siku ya Jumamosi.

Msikiti wa Sahaba ulioko mjini humo ndio unaoandaa hafla hiyo ya kimataifa.

Katika hotuba yake kwa hafla ya ufunguzi, Waziri wa Wakfu Misri Sheikh Mohamed Mukhtar Gomaa alisema mashindano hayo yanalenga kubainisha na kuhimiza watu wenye fikra na vipaji vya kuhifadhi Qur'ani, kukuza utamaduni wa Kiislamu na kueneza fikra za kidini.

Pia inalenga kuwafahamisha washiriki kuhusu uzoefu wa Misri katika kutumikia Kurani Tukufu, alisema.

Khaled Fawda, gavana wa Sharm el-Sheikh, pia alihutubia tukio hilo ambapo alifafanua juu ya umuhimu wa kitamaduni na kihistoria wa Msikiti wa Sahaba na usanifu wake.

Mashindano hayo ya kimataifa yanafanyika kwa hatua mbili, huku washindi wakitarajiwa kupokea zawadi za fedha taslimu kuanzia pauni 100,000 hadi milioni 2.3 za Misri.

4211632

captcha