IQNA

Mwanamke Mwislamu Mcheza Basketboli ataka FIBA iruhusu Hijabu

23:19 - July 23, 2016
Habari ID: 3470469
Mwaka moja uliopita, Indira Kaljo, mwanamke Mwislamu mcheza basketboli, aliamua kuvaa vazi la staha la Kiislamu, Hijabu.
Manamke Mwislamu Mcheza Basketboli ataka FIBA iruhusu Hijabu

Alichukua uamuzi huo wa kuvaa Hijabu kufuatia, ‘mwamko’ alioupata akiwa katika nchi iliyokuwa imekumbwa na mtetemeko wa ardhi ya Haiti, ameripoti mwandishi wa IQNA akinukulu World Bulletin.

Lakini mchezaji huo mwenye asili ya Bosnia na uraia wa Marekani anasema alifahamu kuwa hataweza kuwa mchezaji wa kulipwa barani Ulaya kwa sababu Shirikisho la Kimataifa la Basketboli FIBA imepiga marufuku chochote kinachofunika kichwa ikiwa ni pamoja na Hijabu na vilemba katika michezo rasmi.

"Si sawa,” anasema Kaljo, ambaye anaamini kuwa marufuku hiyo ni ubaguzi kwa wanamichezo wanaotaka kucheza na pia kuendeleza kuzingatia mafundisho ya dini zao, wakiwemo Waislamu, Masingasinga na Mayahudi.

Mwaka 2014, alianzisha kampeni katika intaneti ambapo alifanikiwa kukusanya saini 70,000 na kuwavutian wengi duniani ambapo amanasema anataka FIBA iliegeza msimamo wake mkali na kuruhusu Hijabu. Septemba 2014 FIBA ilitangaza kuwa wanawake Waislamu wanaruhusiwa kuvaa Hijabu katika michezo ya kitaifa kwa muda wa miaka miwili ya majaribio.

FIBA inadai marufuku ya Hijabu inatokana na sababu za usalama wa wachezaji lakini Kaljo, ambaye hivi sasa yuko Uturuki anasema sababu inayotolewa na Fiba si sahihi kwani binafsi anacheza basketboli akiwa amevaa Hijabu bila tatizo lolote.

Mchezaji huyu chipukizi wa basketboli anasikitika kuwa wanawake wengi Waislamu huachana na mchezo huo mara wanapoamua kuvaa Hijabu. Anaongeza kuwa, FIBA inapaswa kuruhusu Hijabu katika michezo ya kimataifa. Kaljo ambaye pia ana shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Activne, ambalo huhusika na kustawisha wanawake Waislamu kupitia michezo anasema, marufuku ya Hijabu katika basketboli kimataifa inapaswa kuondolewa ili wanawake waweze kushiriki katika mchezo huo.

3460466

captcha