IQNA

Warsha ya pili ya mazungumzo baina ya dini yafanyika Zimbabwe+PICHA

21:32 - October 23, 2016
Habari ID: 3470631
IQNA-Warsha ya pili ya kieneo ya mazungumzo baina ya dini imefanyika nchini Zimbabwe kwa himaya ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hulo limewashirikisha wajumbe kutoka Zimbabwe na pia nchi za kigeni zikiwemo Afrika Kusini, Malawi na Zambia. Wasomi wa Kiislamu kutoka madhehebu ya Shia na Sunni na pia wawakilishi wa Ukristo na dinia za kienyeji walishiriki katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na wahadhiri na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe na pia Chuo cha Arrupe (kinachofungamana na Chuo Kikuu cha Kikatoloki cha Zimbabwe.

Katika mkutano wa huo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Arrupe mjini Harare kuanzia Octoba 19-21, Alfred Tomy Mtendaji Mkuu katika mkoa wa Harare amesema amemshukuru Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuandaa warsha hiyo. Amesema ni jambo la kusikitisha kuwa sera za nchi za Magharibi ndio chanzo cha malumbano ya kidini duniani. Aidha amesema kinyume na baadhi ya nchi duniani, wafuasi wa dini mbali mbali na hasa Waislamu na Wakristo nchini Zimbabwe wanaishi kwa amani na maelewano.

Kwa upande wake, Muhsin Shujaakhani, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Zimbabwe amewashukuru wote walioshiriki na kuwasilisha Makala katika warsha hiyo.

Pembizoni mwa warsha hiyo kulikuwa na jarida maalumu la kitaalamu la Mazungumzo Baina ya Dini ambacho hutayarishwa na Kituo cha Kimataifa cha Mazungumzo Baina ya Dini katika Shirika la Iran la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ICRO na pia Kituo cha Kiislamu cha London.

Warsha ya pili ya mazungumzo baina ya dini yafanyika ZimbabweWarsha ya pili ya mazungumzo baina ya dini yafanyika ZimbabweWarsha ya pili ya mazungumzo baina ya dini yafanyika Zimbabwe
Warsha ya pili ya mazungumzo baina ya dini yafanyika Zimbabwe

3540155

captcha