IQNA

Waislamu Malawi wapongeza Tarjuma ya Qur'ani Tukufu Kwa Kiyao

0:09 - March 01, 2017
Habari ID: 3470873
IQNA: Waislamu nchini Malawi wamepongeza tarjuma ya Qur’ani Tukufu kwa lugha ya Kiyao na kisema itawawezesha kufahami vyema zaidi mafundisho ya kitabu hicho kitukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Saad Malovu wa Kituo cha Jeshi cha Kamuzu mjini Lilongwe amesema Waislamu wengi nchini Malawi hawafahamu lugha ya Kiarabu na hivyo hawakuwa wakielewa mafundisho ya Qur’ani ipasavyo. Sheikh Malovu amesema asilimia 60 ya Waislamu nchini Malawi ni wa kabila la Yao na kwa msingi huo kuanzia sasa watafahamu kikamilifu mafundisho ya Qur’ani iliyotarjumiwa kwa lugha wanayoifahamu. Kwa upande wake, Jalafi Ziyabu, mwalimu wa Kiislamu katika mji wa Mangochi amebainisha furaha yake kufuatia kuchapishwa tarjuma ya Qur’ani kwa lugha ya Kiyao.

Qur'ani hiyo ilizinduliwa mwezi Desemba mwaka jana katika sherehe iliyofanyika mjini Mangochi kusini mwa nchi hiyo.

Sheikh Muhammad Abdul-Hamid Silika ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Iftaa la Maulamaa wa Malawi amechukua muda wa miaka 10 kuitarjumu Qur'ani kwa Kiyao kutoka lugha ya Kiarabu.

Wayao ni kabila la Kibantu kutoka eneo la karibu na Ziwa Nyasa barani Afrika ambapo ina wazungumzaji takribani milioni mbili nchini Malawi na nusu milioni Tanzania katika mikoa ya Mtwara na Ruvuma na nusu mwilini wengine nchini Msumbiji.

Aghalabu ya Wayao ni waumini wa dini ya Uislamu na miongoni mwao waliopata umaarufu mkubwa ni pamoja na marais wawili wa zamani wa Malawi Bakili Muluzi pamoja na Joyce Banda.

3462304

captcha