IQNA

Wafanyaziara milioni 1.5 wa kigeni waingia Iraq kwa ajili ya Arubaini

10:14 - November 17, 2016
Habari ID: 3470681
IQNA-Wafanyaziara zaidi ya milioni 1.5 wa kigeni (bila kuhesabu Wairani) wameingia Iraq kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iraq imetangaza kuwa tayari kabisa kuwapokea wafanyazia hara wa Siku ya Arubaini wanaoelekea katika mji wa Karbala. Aidha maafisa wa wizara hiyo wamesisitiza umuhimu wa kuzingatiwa njia rasmi za kuingia Iraq. Aghalabu ya wanaoshiriki katika Ziara ya Siku ya Arubaini, ambayo kilele chake kitakuwa Jumapili na Jumatatu, ni raia wa Iraq.

Tayari kuna wafanyazaira zaidi ya milioni mbili kutoka nchi jirani ya Iran ambao nao pia wameingia Iraq kwa ajili ya ziara hiyo ya kila mwaka. Inatazamiwa kuwa wafanyaziara zaidi ya milioni 22 watashiriki katika Ziara ya Arubaini mwaka hii ambapo ni ongezeko la karibu asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka jana ambapo kulikuwa wafanya ziara zaidi ya milioni 20 waliofika Karbala.

Inafaa kukumbusha hapa kuwa, majlisi na ziara ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria,  baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala.

3546559

captcha