IQNA

Diplomasia ya Kiislamu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Kiongozi wa Hizbullah wakutana Beirut

19:08 - November 24, 2023
Habari ID: 3477936
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza utayarifu kamili wa muqawama katika nyanja mbalimbali na kuutaja ushindi wa mwisho wa muqawama na kushindwa adui Mzayuni kkwamba, ni hakika na jambo lisilo la shaka.

Sayyyid Hassan Nasrullah amesema hayo mjini Beirut Lebanon katika mazungumzo yake na Hussein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kkusisitiza kwamba, ushindi ni wa muqawana na bila shaka adui atashindwa.

Katika mazungumzo hao wawili hao wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusiana na matukio ya hivi punde katika eneo, Lebanon na Palestina na vita vya Gaza na wajibu wa pande zote katika kipindi hiki cha kihistoria na cha hatima ni kuunga mkono suala la Palestina na Quds takatifu na juhudi za sasa za kisiasa za kusimamisha mashambulio ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Katika kikao hicho, Waziri wa Mashauri ya kkigeni wa Iran  alimfahamisha kwa kifupi kuhusu harakati na mashauriano ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika wiki zilizopita kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Palestina na kukomesha jinai za kivita za utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya raia wa Ukanda wa Ghaza.

Kwa upande wake Samahat Seyyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashiria pia kusimama kidete kusiko na mithili kwa wapiganaji wa muqawama na wananchi wanamuqawama wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kusisitiza utayarifu kamili wa muqawama katika nyanja mbalimbali na kusisitiza kwamba, kambi ya muqawama itapata na kushindwa kwa adui wa Kizayuni ndio uhalisia na jambo lisilo na shaka.

3486142

Habari zinazohusiana
captcha