IQNA

OIC yalaani kuzuiwa Waislamu Myanmar kushiriki sensa

17:14 - April 19, 2014
Habari ID: 1397232
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imelaani hatua mpya ya serikali ya Myanmar kuondoa jina jamii ya Waislamu wa Rohingya katika takwimu rasmi za nchi hiyo.

Kwa mujibu  wa mwandishi wa Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA, katika taarifa, Iyyad Madani Katibu Mkuu wa OIC ameelezea wasi wasi wake kuhusu kuondolewa jina la kabila la Waislamu la Rohingya katika fomu za sense nchini Myanmar. Amesema hatua hiyo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa kuhusu sensa. Amesema kitendo hicho cha wakuu wa Maynmar ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binaadamu na haki za raia.
Hivi karibuni pia Umoja wa Mataifa uliikosoa serikali ya Myanmar kwa kukiuka ahadi ilizotoa kutokana na hatua yake ya kuwazuia Waislamu wa nchi hiyo wasishiriki kwenye sensa ya kuhesabu watu. Mfuko wa Sensa ya Jamii wa Umoja wa Mataifa (UNFPA) umetangaza kuwa serikali ya Myanmar iliahidi kuwa katika zoezi hilo la sensa ya kuhesabu watu, itaheshimu na kuzingatia viwango vya kimataifa na misingi ya kisheria. Taarifa ya UNFPA imeeleza kuwa, vizuizi vilivyowekwa kwa ajili ya kushiriki kwenye sena hiyo Waislamu wa kabila la Rohingya, vinaifanya itibari ya sensa hiyo kutiliwa shaka na pia inaweza kupelekea kushadidi kwa hali ya mivutano katika mkoa wa Rakhin.
Sensa ya watu ya kwanza kuwahi kufanyika huko Myanmar katika kipindi cha miongo mitatu iliyopita, ilianza kote nchini humo Jumapili iliyopita na itaendelea hadi tarehe 10 mwezi huu. Serikali ya Myanmar imetangaza kuwa Waislamu wa Rohingya wa nchini humo hawaruhusu kujiandikikisha kwa ajili ya kushiriki kwenye sensa hiyo kwa kujitambulisha kama watu wa kabila la Rohingya. Serikali ya Myanmar haiwatambui rasmi Waislamu wa nchi hiyo na ndio maana hunyamaza kimya bila ya kuwasaidia watu hao mbele ya mashambulizi ya umwagaji damu yanayofanywa dhidi yao na Mabudha wa nchi hiyo wenye misimamo mikali.

1397134

captcha