IQNA

Waislamu Myanmar wangali katika hali mbaya

16:46 - August 09, 2014
Habari ID: 1437511
Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar wangali wanaishi katika hali ngumu na mazingira mabaya na makumi ya maelfu miongoni mwao wanakabiliwa na uhaba wa chakula, maji na huduma za afya.

Ripoti zinasema kuwa serikali ya Myanmar imeendeleza sera zake za ubaguzi dhidi ya Waislamu kwa kuzuia jumuiya za kimataifa za misaada ya kibinadamu kuingia katika maeneo ya Waislamu wa jamii ya Rohingya.

Mwandishi wa Press TV anaripoti kuwa kambi za wakimbizi wa Kiislamu wa Rohingya hazina huduma za afya, maji na mahitaji mengine ya dharura na kwamba serikali ya Myanmar inabana shughuli za jumuiya za misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi hao.

Maelfu ya Waislamu wa jamii ya Rohingwa wanaounda asilimia tano ya watu wa Myanmar wameuawa na maelfu ya wengine kukimbia makazi yao kufuatia mashambulizi yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali wanaosaidiwa na jeshi la serikali. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Waislamu wa Rohingya wa Myanmar ni miongoni mwa jamii zilizodhulumiwa zaidi duniani.

1437393

captcha