IQNA

Ban ataka kuokolewa Waislamu wa Myanmar kuwe kipaumbele

9:45 - May 24, 2015
Habari ID: 3306970
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuhusu umuhimu wa kuokoa maisha ya wakimbizi wa Myanmar walioachwa baharini kusini mashariki mwa Asia.

Aghalabu ya wakimbizi hao ni Waislamu wa kabila la Rohingya ambao wanakimbia Myanmar kutokana na kukandamizwa na kubaguliwa katika nchi hiyo.

Akizungumza siku ya Jumamosi akiwa katika mji mkuu wa Vientam, Hanoi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea amatumaini yake kuwa nchi za eneo zitachunguza sababu haswa iliyopelekea kuibuka wimbi kubwa la wakimbizi katika eneo. Amesema hivi sasa suala ambalo linapaswa kupewa kipaumbele ni kuwasaidia wakimbizi waliokwama baharini na kuwapatia misaada ya dharura ili kuokoa maisha yao. Serikali ya Mabuddha nchini Myanmar inakabiliwa na mashinikizo ya kimataifa kutokana na kuwabagua na kuwakandamiza Waislamu wa kabila la Rohingya nchini humo ambao idadi yao inakadiriwa kuwa milioni moja na laki tatu. Umasikini, ukandamizaji na ubaguzi wa Waislamu hao wanaoishi katika jimbo la Rakhine magahribi mwa Myanmar ndicho chanzo cha kuibuka wimbi kubwa la wakimbizi.  Aghalabu ya wakimbizi hao huelekea katika nchi za Malaysia na Indonesia nchi ambazo sasa zinakataa kuwapokea.../mh

3306688

captcha