IQNA

UN: Waislamu wa Myanmar wanahitaji misaada

11:42 - June 14, 2015
Habari ID: 3314114
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa karibu Waislamu nusu milioni wa jamii ya Rohingya huko Myanmar wanaoendelea kukabiliwa na masaibu wanahitaji misaada ya dharura.

Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Dharura ya Umoja wa Mataifa (UNOCHA) imetangaza kuwa Waislamu laki nne 16 elfu wa jamii ya Rohingya wangali wanahitaji misaada ya dharura ya kibinadamu kufuata miaka mitatu sasa ya machafuko na hujuma za Mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya watu wa jamii hiyo. Ripoti hiyo inasema idadi hiyo inajumuisha Waislamu 140,000 waliofukuzwa katika makazi yao ambao wanaishi katika hali mbaya makambini na wengine wakiishi katika hali ya kutengwa kwenye vijiji vya mbali.
Zaidi ya Waislamu milioni 1.3 wa jamii ya Rohingya huko Myanmar wanasumbuliwa na ubaguzi ikiwa ni pamoja na kudhibiwa harakati zao na kunyimwa ajira. Maelfu ya Waislamu hao wameua na wengine kulazimika kukimbilia katika nchi jirani kutokana na hujuma zinazoendelea kufanywa na Mabudha wenye misimamo mikali wakisaidiwa na vyombo vya dola dhidi ya watu wa jamii ya Rohingya.../mh

3313821

captcha