IQNA

Saad Hariri ateuliwa kwa mara nyingine kuwa Waziri Mkuu wa Lebanon

11:08 - October 23, 2020
Habari ID: 3473287
TEHRAN (IQNA) - Saad Hariri ameteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu wa Lebanon na sasa ametakiwa kuunda serikali yake ya nne, mwaka mmoja baada ya kuachia ngazi.

Hariri ambaye alipendekezwa kuchukua wadhifa huo kufuatia mashauriano ya Rais Michel Aoun na viongozi wa mirengo kadhaa ya Bunge la nchi hiyo ya Kiarabu, ameteuliwa katika wadhifa huo baada ya kupata ushindi mwembamba wa kura 65 bungeni.

Waliojizuia kupiga kura katika zoezi hilo ni wabunge 53 wa mirengo tofauti ya kisiasa nchini humo.

Hariri anakuja kurithi mikoba ya Mustapha Adib ambaye alitangaza kujiuzulu wadhifa wake huo mwishoni mwa mwezi uliopita, baada ya kushindwa kuunda serikali.

Oktoba 17 mwaka jana, Lebanon ilianza kushuhudia maandamano ya wananchi ambayo yalipelekea kujiuzulu kabla ya wakati Saad Hariri.

Mbali na Hariri, Hassan Diyab na Mustafa Adib ni mawaziri wakuu wengine ambao Lebanon imekuwa nao ndani ya muda wa mwaka mmoja.

Mbali na migogoro ya kisiasa na janga la corona, nchi hiyo ya Kiarabu inaandamwa pia na misukosuko ya kiuchumi.

3472906

Kishikizo: HARIRI lebanon uchaguzi
captcha