IQNA

Qur'ani Tukufu

Uelewa wa kina wa mafundisho ya Qur’ani ni lazima kwa waalimu wa Qur’ani

22:31 - December 23, 2023
Habari ID: 3478079
IQNA - Haitham Salim Ayyash, mtaalamu wa Qur'ani wa Lebanon, alisisitiza haja ya walimu wa Qur'ani kuwa na ufahamu wa kina wa mafundisho ya Kitabu hicho Kitukufu.

Akizungumza na mwandishi wa IQNA nchini Lebanon Rima Fares, Ayyash amesema walimu wa Qur'ani lazima pia wawe na uwezo mkubwa wa kufikisha maadili ya kidini na akhlaqi.

Aidha alisema, kufundisha sayansi za Qur'ani kunahitaji ufahamu wa kina wa Sharia ya Kiislamu.

Ayyash, ambaye anatoka katika mji wa Nabatieh Kusini mwa Lebanon, alisema kwamba katika utoto wa mapema, alipata shauku ya kusikiliza visomo vya Qur'ani vya maqari mashuhuri.

Kisha akajiunga na Taasisi ya Dawah na Irshad Qur'ani kujifunza Qur'ani na kupata ruhusa ya kusoma Qur'ani.

Pole pole, aliboresha ujuzi wake wa Kurani na kuanza kufundisha Qur'ani na kuhudumu kama jaji katika uwanja wa Lahn na Ibtida katika mashindano ya Qur'ani.

Amesema kozi za Qur'ani zinazoandaliwa na Taasisi ya Dawah na Irshad nchini Lebanon zinasaidia kukuza utamaduni wa Qur'ani katika jamii.

Kufundisha usomaji wa Kurani, Lahn na tafsiri huwasaidia wanafunzi kuelewa vyema Kitabu Kitakatifu, Ayyash aliongeza.

4189044

Kishikizo: qurani tukufu lebanon
captcha