IQNA

Kiongozi Muadhamu: Shahidi Soleimani alikuwa shakhsia mkubwa zaidi Iran, Umma wa Kiislamu

18:00 - January 01, 2022
Habari ID: 3474753
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), ndiye shakhsia mkubwa zaidi si tu ndani ya Iran, bali katika Umma wote wa Kiislamu.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo Jumamosi wakati alipokutana na familia ya Shahidi Soleimani,  kwa mnasaba wa kuwadia mwaka wa pili tangu alipouawa shahidi shujaa huyo wa kupambana na ugaidi.

Ayatullah Khamenei ameeleza kuwa, hii leo mrengo wa muqawama au mapambano ya Kiislamu umeimarika zaidi na kupata matumaini makubwa kuliko ilivyokuwa miaka miwili iliyopita, kutokana na kuuawa shahidi jenerali huyo anayeenziwa na wote.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema sifa alizojipamba nazo Shahidi Soleimani kama ya ukweli na uaminifu, zilimpelekea mwanamuqawama huyo awe kigezo na kielelezo chema kwa vijana wa eneo la Asia Magharibi.

Ayatullah Khamenei amesema, "hii leo, Jenerali kipenzi Soleimani, kutokana na jitihada zake, amekuwa nembo ya matumaini, kujiamini, ushujaa, uvumilivu na ushindi katika eneo."

Kiongozi Muadhamu amemtaka Shahidi Soleimani kuwa ni  "ukweli wenye kudumu' huku wauaji wake kama vile rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na wengine kama yeye watasahauliwa na watapotea katika jaa la taka za historia, na hilo litafanyika baada ya kuwa wamelipa gharama za jinai zao hapa duniani."

Shahidi Soleimani ambaye Januari 3 mwaka 2020 alielekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo, aliuliwa shahidi akiwa pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Mkuu wa jeshi la kujitolea la wananchi wa Iraq la al Hashdu-Sha'abi na wanajihadi wengine wanane katika shambulio la kikatili la jeshi la kigaidi la Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.

4025113

captcha