IQNA

Ibada ya Hija

Wakuu wa Hilali Nyekundu za Iran, Saudia wajadili ushirikiano katika Hija

15:20 - July 11, 2022
Habari ID: 3475487
TEHRAN (IQNA) – Marais wa Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran (IRCS) na Mamlaka ya Hilali Nyekundu ya Saudia wamekutana mjini Mina mkoani Makka Jumapili, kujadili ushirikiano wa pande mbili.

Rais wa IRCS Dkt. Pir-Hossein Kolivand aliwaambia waandishi wa habari kwamba alikutana na Dkt. Jalal Bin Mohammed Al-Owaisi huko Mina wakati mahujaji wanatekeleza ibada za mwisho za za Hija mwaka huu.

Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano huo, Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran inaweza kutumia vifaa na suhula za Mamlaka ya Hilali Nyekundu ya Saudia wakati wa kutoa huduma kwa mahujaji, Kolivand alisema.

Kwa mfano, wale Mahujaji ambao wanapaswa kurudi Iran kutokana na dharura za hali ya afya watafikishwa aktika Uwanja wa Ndege wa Jeddah kwa ambulensi za Saudia.

Saudi Arabia pia itatoa kwa upande wa Irani vifaa vyote vya matibabu vinavyohitajika, aliongeza. Huduma hizi zote zitatolewa kwa njia ya “kidugu, kirafiki,” alisisitiza Kolivand.

Iran tayari imeanzisha vituo kadhaa vya matibabu huko Makka na Madina ili kuwahudumia Mahujaji.

Mahujaji milioni moja kutoka nchi mbalimbali wametekeleza ibada ya Hija mwaka huu baada ya miaka miwili ya vikwazo kutokana na janga la virusi vya corona.

Iran imetuma zaidi ya Mahujaji 39,000 nchini Saudi Arabia kushiriki katika ibada ya Hija mwaka huu na wote wamefika katika ufalme huo kwa kutumia Shirika la Ndege la Iran. Mahujaji Wairan wanatazamiwa kuanza kurejea nyumbani Julai 14.

3479653

captcha