IQNA

Hossein Amir Abdollahian

Iran kuendeleza mazungumzo na Saudi Arabia

22:27 - March 27, 2022
Habari ID: 3475080
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Iran iko tayari kwa ajili ya duru ya tano ya mazungumzo na Riyadh.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir Abdollahian ameiambia televisheni ya Al-Mayadeen kwamba uhusiano Iran na Saudi Arabia sio mzuri, lakini Iran haihusiki na suala hili, na tumetangaza utayarifu wetu kwa ajili ya duru ya tano ya mazungumzo na Riyadh."

Amir Abdollahian ameongeza kuwa: Uhusiano wa Iran na Saudi Arabia unakabiliwa na matatizo na changamoto na tunafanya kazi kwa bidii ili kubakisha wazi milango ya mazungumzo kati ya pande mbili.

Akiashiria kwamba Saudi Arabia ilikuwa ya kwanza kukata uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Tehran ina uhusiano mwema na nchi nyingine za Kiarabu kama Kuwait na Imarati.

Amesema Tehran haikubaliani na baadhi ya siasa na sera za serikali ya Riyadh lakini hata hivyo haikukata uhusiano wake na Saudia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa: "Baadhi ya mienendo inayokinzana na isiyofaa ya Saudi Arabia, ikiwa ni pamoja na kuwanyonga watu 81, zinaathiri uhusiano na nchi hiyo na Iran. 

Amir Abdollahian ameeleza kuwa Wasaudi hawataki kuwa na uhusiano mwema na Iran kuongeza kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu haitasahau kuuawa shahidi mahujaji 460 wa Iran katika tukio la Mina."

4044999

captcha