IQNA

Mapambano ya Kiislamu

Mwanazuoni wa Kiislamu wa Lebanon asifu nafasi ya Iran katika Mhimili wa Muqawama

23:08 - September 13, 2022
Habari ID: 3475779
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya al-Umma ya Lebanon Sheikh Abdullah al-Jabri amepongeza nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mhimili wa muqawama au mapambano ya Kiislamu.

Akizungumza katika mkutano na Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Lebanon Seyed Komeyl Baqerzadeh, Sheikh Jabri alisema Iran ni mwanachama wa juu wa mhimili wa upinzani.

Kwa kuzingatia miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Iran inakabiliana na vitisho kwa muqawama na kusimama kidete.

Sheikh Jabri pia alisifu mafanikio na ushindi wa Iran dhidi ya madora yenye kiburi au ya kiistikbaru duniani, Uzayuni na tawala zinazopinga mabadiliko.

Katika mkutano huo, afisa huyo wa Iran na mwanasiasa huyo wa Lebanon walijadili maendeleo ya kieneo na masuala ya kiutamaduni na kiakili.

Walisisitiza haja ya juhudi za kufikia malengo ya pamoja ya Kiislamu, hasa katika masuala ya kuendeleza mafundisho ya Uislamu.

Walisema hili lifanyike kwa kuzingatia umoja na kuamurisha mema na kukataza maovu.

 Mhimili wa Muqawama unajumuisha  Iran, Syria, na harakati za mapambano hasa  Hizbullah, Hamas, Jihad Islami, Ansarullah na makundi mengine ya muqawama katika eneo.

4085202

captcha