IQNA

Kadhia ya Palestina

Naibu Mkuu wa Hizbullah: Watu wa Palestina wataibuka na nguvu zaidi katika vita vya Gaza

20:28 - December 03, 2023
Habari ID: 3477980
TEHRAN (IQNA) - Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema watu wa Palestina wataibuka katika vita dhidi ya Gaza wakiwa na nguvu zaidi kuliko hapo awali.

Sheikh Naim Qassem amesema utawala wa Kizayuni hauna uwezo wa kusambaratisha kadhia ya Palestina kupitia uvamizi wake katika Ukanda wa Gaza.

Amesema vikosi vya muqawama (mapambano ya Kiisalmu)  vitabaki thabiti na kumkatisha tamaa adui.

Mwanazuoni huyo amesisitiza kuwa, utawala ghasibu wa Israel haujafanikiwa chochote katika hujuma zake za siku 50 za Ukanda wa Gaza.

Hata askari wao walioshikiliwa na wapigania ukombozi wa Palestina waliachiliwa kwa kubadilishana wafungwa baada ya usitishaji vita.

Vita ambavyo Israel imeanzisha vitakuwa kwa madhara yake, alisema.

Sheikh Qassem aliongeza kuwa Wapalestina wataibuka na nguvu zaidi kutokana na vita hivi huku Israel ikidhoofika zaidi.

Vile vile amesisitiza uhusiano kati ya vikosi vya muqawama vya Palestina na Lebanon na kusema Hizbullah itafikisha msaada wowote ambao ni muhimu kwa wapigania ukombozi wa Palestina katika kupata ushindi dhidi ya adui.

Israel ilianzisha vita dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba kujibu operesheni ya ghafla iliyopewa jina la Kimbunga cha Al-Aqsa na iliyotekelezwa na harakati ya muqawama wa Palestina, Hamas. Hili lilikuwa ni jibu kwa kampeni ya miongo kadhaa ya utawala wa Israel ya umwagaji damu na uharibifu dhidi ya Wapalestina.

Kulingana na wizara ya afya yenye makao yake makuu mjini Gaza, zaidi ya Wapalestina 15,500, wakiwemo zaidi ya watoto 6,500 na wanawake 4,000, wameuawa katika mashambulizi ya Israel. Wengi zaidi wanahofiwa kuwa chini ya vifusi Utawala haramu wa Israel unaendelea kulaaniwa duniani kote.

3486264

Habari zinazohusiana
captcha