IQNA

Wasomaji maarufu wa Qur'ani Tukufu Misri wakisoma aya ya tano ya Surat Al-Isra + video

Katika kuunga mkono operesheni ya "Kimbunga cha Al-Aqsa" inayotekelezwa Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina, Shirika la Habari la Kimataifa la Habari la Qur'ani la Iran, IQNA, imetayarisha klipu ya wasomaji Qur'ani Tukufu wa Msri wakiwa wanasoma aya ya tano ya Surat Al-Isra.

Aya ya tano ya Surat al-Isra inasema hivi: Basi itapo fika ahadi ya kwanza yake tutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita. Watakuingilieni ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyo timizwa."

Klipu ya qiraa hii ambayo IQNA ina sauti ya Mashekhe watano maarufu wa Misri (Mwenyezi Mungu awarehemu wote), ambao ni Sheikh Muhammad Siddiq Al-Minshawi, Sheikh Mustafa Ismail, Sheikh Abdul Basit Abdul Samad,  Sheikh Mahmoud Ali Al-Banna na Sheikh Kamel Yusuf Al-Bahtimi.