IQNA

Jinai za Israel

Ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya Watoto waoongezeka katika vita vya Israeli dhidi ya Gaza

13:37 - November 02, 2023
Habari ID: 3477828
GENEVA (IQNA) - Kamati ya haki za watoto ya Umoja wa Mataifa imeonya kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watoto katika vita vinavyoendelea vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Gaza, ikilaani vikali mauaji yanayotekelezwa na utawala huo dhidi watoto katika vita hivyo vya kikatili.

Kamati hiyo yenye makao yake makuu mjini Geneva ililaani ongezeko la mashambulizi ya Israel dhidi ya maeneo ya kiraia katika Ukanda wa Gaza, ambao ambayo yamepelekea watoto wasiopungua 3,600 wa Kipalestina kupoteza maisha tangu tarehe 7 Oktoba.

"Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watoto unaongezeka kwa dakika katika Ukanda wa Gaza, na hakuna washindi katika vita ambapo maelfu ya watoto wanauawa," kamati hiyo imesema.

Tangu kuanza kwa hujuma hiyo, utawala wa Tel Aviv umekuwa ukifanya jinai za kivita huko Gaza na kuwaua Wapalestina wasiopungua 8,800 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na kuwajeruhi wengine zaidi ya 23,000.

Wataalamu huru wa haki za binadamu wa kamati ya Umoja wa Mataifa walisema kumekuwa na "ripoti mbaya za vitendo ambavyo vinakatazwa na sheria ya kimataifa ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na kulemaza, kujeruhiwa, kutekwa nyara, kuhamishwa kwa nguvu, kunyimwa huduma za matibabu, chakula na maji".

Walitoa wito kwa pande zote kuwalinda watoto wote na kuwapa msaada unaohitajika wa kiafya na kisaikolojia.

"Kusitishwa kwa mapigano kunapaswa kuwa mwanzo wa majadiliano yanayolenga kuweka amani ya haki na ya kudumu katika kanda ili watoto wote waweze kufurahia haki zao zote kikamilifu," kamati ya Umoja wa Mataifa ilisema.

Wakati huo huo, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA, Martin Griffiths amesema eneo la Wapalestina la Gaza limegeuka kuwa makaburi kwa watoto kwani maelfu wameuawa kufuatia mashambulizi yanayofanywa na utawala haramu wa Israel, huku zaidi ya watoto milioni moja wakikabilwa na uhaba wa mahitaij muhimu na maisha yao ya baadaye yakiwa mashakani.

Ofisi ya OCHA nayo imeripoti kuwa watoto wengine 1,000 Ghaza hawajulikani waliko na pengine wamenasa au wamefukiwa wakiwa tayari wamekufa kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa kwa mashambulizi.

Msemaji wa OCHA, Jens Laerke amesema kuwa “hili ni jambo ambalo haliwezi kuvumilika kufikiria kuwa watoto wamezikwa chini ya vifusi huku kukiwa na uwezekano mdogo kabisa wa kuwanasua.”

Takwimu zilizoripotiwa na shirika la misaada la Save the Children zinaonyesha idadi ya watoto waliouawa katika Ukanda wa Gaza kutokana na uvamizi unaoendelea wa Israel imepita takwimu za kila mwaka zinazohusiana na migogoro ya kimataifa katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

348584

Habari zinazohusiana
captcha