IQNA

Watetezi wa Palestina

Al Azhar: Dunia iungane kuanzisha taifa huru la Palestina

17:02 - November 30, 2023
Habari ID: 3477968
CAIRO (IQNA) - Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimesema wakati umefika kwa watu wote wanaopenda uhuru duniani kuungana kwa ajili ya kuundwa taifa huru la Palestina ili kukomesha ubeberu na ukaliaji mrefu zaidi wa ardhi ya wengine katika historia.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, Al-Azhar ilisisitiza kwamba ulimwengu lazima uungane na kufanya juhudi kwa ajili ya kuunda taifa huru la Palestina.

Al-Azhar ilisisitiza uungaji mkono wake kwa watu wa Palestina katika kutetea kadhia yao.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa Wapalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza wamekuwa wakiteseka kutokana na mauaji ya halaiki yanayotekelezwa na utawala katili wa Israel, kuzingirwa kwake eneo hilo la pwani, kulenga raia na kushambulia hospitali, misikiti, makanisa na shule.

Pia ilibainisha kuwa zaidi ya Wapalestina 15,000, wakiwemo watoto 6,000 na wanawake 5,000, hadi sasa wameuawa katika mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

3486232

Taarifa hiyo iliwasifu watu wanaopenda uhuru duniani kwa kujitokeza mitaani katika miji mbalimbali duniani kutoa sauti ya mshikamano wao na watu wa Palestina, na kuwataka waendelee na juhudi zao za kukomesha ukiukaji, uchokozi na vikwazo vya Israel dhidi ya Gaza.

Mipango, mikutano na sherehe mbalimbali zilifanyika katika nchi tofauti siku ya Jumatano kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina.

Tarehe 29 Novemba 1947 ni siku ambapo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kuigawanya Palestina.

Hivyo 29 Novemba imekuwa ikiadhimishwa Kama Siku Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina tangu 1978.

Mwaka huu, siku hii imeadhimishwa huku kukiwa na mauji ya kimbari yanayotekelezwa na Israel dhidi ya Wapalestina  kwenye Ukanda wa Gaza.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: al azhar gaza palestina
captcha