IQNA

Ukandamizaji Saudia

Msomaji wa Qur'ani Saudia afungwa jela kwa miaka 12

13:08 - October 20, 2022
Habari ID: 3475958
TEHRAN (IQNA) - Mahakama ya Ufalme Saudi Arabia imemhukumu mmoja wa wasomaji Qur'ani maarufu wa ufalme huo na mwanaharakati wa kisiasa kifungo cha miaka 12 jela.

Kwa mujibu wa ripoti ya akaunti ya Twitter ya Wafungwa wa Kiitikadi, mahakama ya Saudi ambayo inashughulikia kesi zinazohusiana na 'ugaidi' ilitoa hukumu hiyo kwa Sheikh Abdullah Basfar.

Amepewa kifungo cha jela kwa kukubali kuwa Imamu wa Sala katika Msikiti wa Hagia Sophia mjini Istanbul, Uturuki, miaka minane iliyopita.

Hakuna maelezo zaidi kuhusu hukumu hiyo.

Sheikh Basfar alizuiliwa mnamo Agosti 2020 wakati wa ukandamizaji dhidi ya wapinzani, wanaharakati wa haki, wanaharakati wa kisiasa na wasomi huko Saudi Arabia.

Sheolj Basfar ni msomaji mashuhuri wa Qur'ani ambaye pia aliwahi kufundisha sayansi ya Kiislamu katika chuo kikuu cha Jeddah na aliwahi kuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Qur'ani na Sunnah kwa miaka kadhaa.

Amir al-Muhalhal ni Qarii mwingine maarufu wa Qur'ani ambaye aliwekwa chini ya ulinzi wakati wa ukandamizaji wa Agosti 2020.

Tangu Mrithi w Kitu cha Ufalme Mohammed bin Salman awe kiongozi mkuu asiye rasmi wa Saudi Arabia mnamo 2017, ufalme huo umewakamata mamia ya wasomi wa Kiislamu, wanaharakati, wanablogu, wasomi na wengine kwa harakati zao za kisiasa.

4091760

captcha