IQNA

Jinai za Saudia

Daktari Mtunisia afungwa jela miaka 15 Saudia kwa kuunga mkono Hizbullah

10:40 - October 23, 2022
Habari ID: 3475975
TEHRAN (IQNA)- Saudi Arabia imemfunga jela miaka 15 daktari mmoja wa kike raia wa Tunisia kwa kuweka video ya maandamano ya kuiunga mkono Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon huko Tunisia.

Kwa mujibu wa televisheni ya Al Mayadeen, mahakama moja nchini Saudia imemuhukumu kifungo cha miaka 15 jela Daktari Bi Mahdia al-Marzouki  kwa madai ya kuuvunjia heshima utawala wa kifalme Saudi Arabia. Kosa pekee lililofanywa na daktari huyo raia wa Tunisia ni kuweka kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, video ya maandamano ya wananchi wa Tunisia waliokuwa wanaunga mkono Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.

Televisheni ya al Mayadeeni imemnukuu kaka wa daktari huyo akisema kuwa, dada yake mwenye umri wa miaka 51, amekuwa akiishi nchini Saudia tangu mwaka 2008 kwa ajili ya kufanya kazi ya udaktari. Askari usalama wa ukoo tawala wa Aal Saud walimkamata mwaka 2020 kwa kuweka kwenye ukurasa wake wa Twitter, maandamano ya wananchi wa Tunisia ya kuiunga mkono Hizbullah ya Lebanon.

Daktari huyo amemtaka Rais Kais Said wa Tunisia na wanadiplomasia wa nchi yake wawashinikize watawala wa Saudia wamuachilie huru.

Tangu Mrithi w Kitu cha Ufalme Mohammed bin Salman awe kiongozi mkuu asiye rasmi wa Saudi Arabia mnamo 2017, ufalme huo umewakamata mamia ya wasomi wa Kiislamu, wanaharakati, wanablogu, wasomi na wengine kwa harakati zao za kisiasa ambazo zinakinzana na mitazamo ya ufalme huo wa kiimla.

3480953

captcha