IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Chuo Kikuu cha Jordan Chaandaa Semina ya Qur'ani Tukufu

21:04 - December 14, 2022
Habari ID: 3476249
TEHRAN (IQNA) – Semina ya pili ya Qur’ani ya Chuo Kikuu cha Kiarabu cha Amman katika mji mkuu wa Jordan ilifanyika katika kitivo cha teolojia ya Kiislamu cha chuo hicho.

Sheikh Ahmed al-Nufais, imamu na mhubiri wa Msikiti Mkuu wa Kuwait, ambaye pia ni msomaji mashuhuri wa Qur'ani Tukufuu, alikuwa miongoni mwa washiriki.

Semina hiyo ilianza kwa usomaji wa aya za Qur'an Tukufu na qari wa Kambodia Salehin Muslim, ambaye ni mwanafunzi katika kitivo hicho.

Kisha, Abdullah Abu Shawar, mhadhiri katika chuo kikuu hicho, akazungumza kuhusu hadhi muhimu ya Quran miongoni mwa Waislamu.

Pia alisema vitivo vya teolojia ya Kiislamu vinapaswa kusaidia wahifadhi Qur'ani katika jamii, haswa miongoni mwa kizazi kipya.

Amesema Chuo Kikuu cha Kiarabu cha Amman ni muungaji mkono wa Qur'ani Tukufu na wanaharakati wa Qur'ani na kinaendelea kuwakaribisha wasomaji wa Qur'ani kutoka Jordan na nchi nyinginezo.

Al-Nufais, katika hotuba yake, alisisitiza ulazima wa kuzingatia kuinua vizazi vya Qur'ani na kufanyia kazi mafundisho na amri za Qur'an.

Semina hiyo pia ilijumuisha idadi ya programu za Quran na kidini. Chuo Kikuu cha Kiarabu cha Amman ni chuo kikuu cha kibinafsi huko Amman na ni miognoni mwa vyuo vyenye kuwavutia wanafunzi wengi wa kigeni nchini humo.

 

3481673

captcha