IQNA

Watetezi wa Palestina

'Messi wa Jordan' anajulikana kwa misimamo yake ya kuiunga mkono Palestina

23:07 - February 07, 2024
Habari ID: 3478318
IQNA - Mashabiki wa soka wanamtaja Mousa Mohammad Mousa Sulaiman Al-Tamari kama "Messi wa Jordan".

Ni mmoja wa wachezaji walioisaidia Jordan kufika hatua ya fainali ya Kombe la AFC la Asia 2023 ambalo fainali zake zitachezwa Jumamosi baina ya wenyeji Qatar na Jordan.

Mousa ameifungi timu yake ya taifa mabao mawili katika michuano hiyo na kuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya timu hiyo.

Yeye ndiye mchezaji wa kwanza wa mpira wa miguu wa Jordan katika ligi kuu ya Ufaransa, kwa sasa anaichezea Montpellier.

Mousa ambaye amehifadhi Qur’ani Tukufu, anajulikana barani Ulaya kwa kujitolea kwake katika maadili na kanuni za kidini na kwa misimamo yake ya mshikamano na Palestina.

Anatilia maanani sana kusoma Qur’ani Tukufu na kabla ya kuingia uwanjani, husoma aya za Kitabu Kitukufu na husali kwa wakati.

  Tangu utawala haramu wa Israel uanzishe vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Gaza Oktoba 7 mwaka jana, Mousa amekuwa na msimamo thabiti katika kuunga mkono Palestina.

Hii ni wakati kumekuwa na shinikizo kutoka kwa vyombo vya habari vya Ufaransa kuhusu misimamo yake inayounga mkono Palestina.

 4198277

captcha