IQNA

Hali ya Afghanistan

Al-Azhar: Hatua ya Taliban kuwazuia wanawake kusoma vyuo vikuu ni kinyume cha sheria za Kiislamu

20:54 - December 23, 2022
Habari ID: 3476290
TEHRAN (IQNA) – Sheikhe Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri ameutaka utawala wa Taliban kuondoa marufuku ya elimu ya juu kwa wanawake nchini Afghanistan.

Sheikhe Mkuu wa Al-Azhar , Sheikh Ahmed El-Tayeb Al-Azhar amesema  amesikitishwa sana na uamuzi wa Taliban wa kuwapiga marufuku wanawake wa Afghanistan kutoendelea na masomo ya chuo kikuu.

Katika taarifa yake siku ya Alhamisi, Sheikh El-Tayeb alisema marufuku iliyowekwa na Taliban kwa masomo ya chuo kikuu ya wanawake inakinzana na wito wa Sharia ya Kiislamu kwa wanaume na wanawake kutafuta elimu "kutoka utotoni hadi kaburini".

Al Azhar ni kituo kikuu cha Kiislamu katika Ahul Sunna.

Aidha Sheikh El- Tayeb amebainisha  zaidi kuhusu idadi kubwa ya Hadithi za  Mtume Mohammad SAW kuhusiana na suala hili na kuongeza kuwa kuna  wanawake wengi wa Kiislamu ambao  wamefanikiwa na kuweza kuongoza katika nyanja za sayansi, elimu, na siasa.

"Uamuzi huu wa kushtua kwa dhamiri za Waislamu na wasio Waislamu haukupaswa kutolewa na Mwislamu yeyote," Sheikh Mkuu wa Al Azhar alisema.

Sheikh EL-Tayeb alitoa wito kwa wale walio madarakani nchini Afghanistan kupitia upya uamuzi huo, na kuwakumbusha kuhusu siku ya kiyama  wakati pesa, mamlaka, hadhi na siasa hazitakuwa na manufaa

Mapema wiki hii, Taliban ilitangaza kupiga marufuku mahudhurio ya wanawake katika vyuo vikuu nchini Afghanistan, uamuzi ambao umelaaniwa vikali duniani kote.

Waziri wa Elimu ya Juu wa Taliban Neda Mohammad Nadeem alisema marufuku hiyo imekuja kwa kuwa wanawake hawajatii kanuni za mavazi na kwa kuwa baadhi ya masomo ya shule hayakuwafaa.

3481790

captcha