IQNA

Shahidi Qassem Soleimani

Msafara wa Qur'ani katika kumbukizi ya kuuawa Shahidi Jenerali Soleimani

11:20 - December 30, 2022
Habari ID: 3476328
TEHRAN (IQNA) - Msafara wa Qur'ani uliopewa jina la 'Luteni Jenerali Qassem Soleimani', aliyekkuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), umezinduliwa kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi kamanda huyo aliyeongoza vita dhidi ya ugaidi katika eneo la Asia Magharibi.

Katibu wa Makao Makuu kwa ajili ya kuadhimisha miaka mitatu ya kuuawa shahidi Luteni Jenerali Soleimani, Hujjatul Islam Mohammad Reza Shafiei, alisema msafara huo unajumuisha baadhi ya wasomaji mashuhuri wa Qur'ani nchini Iran

Msafara huo utakuwa na vikao vya Qur'ani Tukufu katika miji kadhaa ya Iran, ikiwa ni pamoja na Tehran, Yazd, Kashan, Naeen, Ardakan, na Kerman, alibainisha.

Ameongeza kuwa, msafara huo utawasili Kerman siku ya Jumamosi ili kushikilia duru ya Qur'ani na kusoma Fatiha kwenye kaburi la Shahidi Soleimani mkoani humo

Jeshi la Marekani liliwaua kigaidi Jenerali Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis, naibu mkuu wa Hashd Al-Shaabi au Jeshi la Kujitolea la Wananchi wa Iraq (PMF) waliuawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mnamo Januari 3, 2020. Shambulizi hilo liliamriwa moja kwa moja na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump. 

Vikao mbalimbali vimepangwa kuandaliwa nchini Iran, Iraq na nchi nyingine kadhaa ili kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Jenerali Soleimani, al-Muhandis na wanamapambano waliokuwa wameandamana nao.

4110465

captcha