IQNA

Mhimili wa Muqawama

Mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Kiongozi wa Hizbullah mjini Beirut

22:15 - April 29, 2023
Habari ID: 3476931
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana Ijumaa alionana na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrullah na kujadiliana naye masuala muhimu ya pande mbili, ya kieneo na ya kimataifa.

Mazungumzo hayo baina Hossein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran na Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon yamehusu masuala mbalimbali ya kisiasa, kieneo na kimataifa na hususan makubaliano baina ya Iran na Saudi Arabia pamoja na matukio ya hivi karibuni ya Lebanon na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. 

Kabla ya hapo Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran alikuwa amezungumza kwa simu na Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS, ambapo harakati hiyo imelishukuru taifa na serikali ya Iran kwa kuliunga mkono muda wote taifa linalodhulumiwa la Palestina.

Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, katika mazungumzo hayo ya simu baina ya Hossein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Yahya Sinwar, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS katika Ukanda wa Ghaza, pande hizo mbili zimepeana mkono wa IdulFitr na kutilia mkazo udharura wa kuzidi kuimarishwa uhusiano baina yao.

Yahya Sinwar amemshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, serikali na wananchi wa Iran kwa uungaji mkono wao wa kisiasa kwa taifa la Palestina.

 

4137061

captcha