Mnamo tarehe 16 Septemba 1982, jeshi la Kizayuni lililokuwa limevamia na kukalia kwa mabavu mji mkuu wa Lebanon, Beirut, lilifanya moja ya mauaji makubwa ya umwagaji damu na ukatili mkubwa zaidi wa karne ya 20 katika kambi mbili za Wapalestina za Sabra na Shatila.
Katika mauaji ya Wapalestina waliokuwa wakiishi kwenye kambi za wakimbizi za Sabra na Shatila, yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu (Septemba 16, 17, 18) na kuongozwa na Ariel Sharon (kwenye picha), waziri mkuu wa utawala wa Israel wakati huo, zaidi ya wakazi elfu tatu wa kambi hizo waliuawa shahidi.
Katika kumbukumbu ya mauaji hayo ya kinyama ya Sabra na Shatila yaliyofanywa na askari wa utawala wa Kizayuni, Nasser Kanani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: "Leo (Jumamosi, Septemba 16) ni siku ya kumbukumbu ya mauaji ya kikatili na kinyama ya wanawake, watoto na wanaume wa Kipalestina wasio na hatia na wasio na ulinzi katika kambi za Sabra na Shatila yaliyofanywa na Wazayuni na mamluki wao, ambao kwa jinai hiyo kubwa waliyofanya, wamewatakasa wahalifu na watendajinai wote katika historia".
Kanani Chafi amesema: "mauaji ya Sabra na Shatila ni doa la aibu na fedheha ambalo halitafutika katu kwenye mapaji ya nyuso za utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake".
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran aidha ameandika: "mauaji ya kikatili na kinyama ya Sabra na Shatila ni mfano mmoja tu wa matendo ya kigaidi yaliyopangwa na kuratibiwa na utawala wa kinyama wa Israel dhidi ya raia wa Palestina wakiwemo watoto, wanawake na wanaume wasio na hatia, kwa sababu jinai hizi zimekuwa zikifanywa kwa miongo mingi na zinaendelea kufanywa kwa uungaji mkono wa Marekani na Ulaya kwa Wazayuni wanaokalia ardhi kwa mabavu".
4169203